Hukumu inayomkabili balozi wa zamani wa Tanzania nchini Italia, Profesa Ricky Costa Mahalu (63) iliyokuwa ikitarajiwa kutolewa leo na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhusiana na kesi ya kuisababishia serikali hasara ya Euro 2,065,827.60 imeahirishwa hadi Agosti 9, mwaka huu.
Kessi hiyo imeahirishwa na Hakimu Katemana, wakati akitoa sababu kuwa ni kukosekana kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi, llivin Mgeta, aliyekuwa akiisikiliza kesi hiyo, ambapo leo amekosekana Mahakamani hapo kwavile ana majukumu mengine ya kikazi.
Awali, katika kesi hiyo, upande wa mashtaka unaoongozwa na mawakili waandamizi wa serikali, Ponsiano Lukosi, Vincent Haule na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ben Linkolin, uliita mashahidi saba na vielelezo tisa vikiwemo mikataba miwili ya ununuzi wa jengo la ubalozi jijini Rome, Italia na upande wa utetezi uliita mashahidi watatu, akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa.
No comments:
Post a Comment