Katika tukio la utambulishaji wa jezi mpya za Manchester City, watengenezaji wa jezi hizo kampuni ya Umbro walifanya mahojiano na wachezaji kadhaa wa timu hiyo, ofcourse interview ya Mario Balotelli ikawa ndio kivutio zaidi.
Alianza kwa kwanza kuzisifia jezi mpya na kuelezea kwanini anapenda kuvaa jezi namba 45. Baada ya hapo akazungumzia jinsi anavyomkubali mwanamuziki Drake ambaye alipigwa naye picha akila nae lunch miezi kadhaa iliyopita, na baada ya hapo akatokea kituko kingine kama ilivyo kawaida yake, aliposema kwamba asingekuwa mcheza soka basi mchezo wa kickboxing ndio ungemfaa zaidi.
"Labda ningekuwa mcheza kickboxing ...... ndio. Naupenda sana mchezo ule," anasema huku akiwa serious.
No comments:
Post a Comment