Thursday, July 26, 2012

NI DAR YANGA AFRICAN NA AZAM FC KAGAME CUP FAINALI JUMAMOSI

 Kikosa cha Yanga kilichoifunga APR ya Rwanda kwa bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Kagame .  Na sasa  watapambana na ndugu zao Azam kuakikisha kombe la Kagame lina bakia Tanzania.


 Kikosi cha Azam kilicho ichapa As Vita club 2 kwa 1 na kuingia fainali za Kagame Cup kwa mala ya kwanza sasa wanakutana na Yanga fainali jumamosi.

Said Bahanuzi 'Spider Man' akiwa amembeba Kiiza baada ya kufunga bao la 'dhahabu'

BAO pekee la mwanasoka bora wa Uganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ dakika ya 110, jioni hii limeipa Yanga tiketi ya kucheza Fainali ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kwa mara ya pili mfululizo, na sasa itamenyana na Azam FC keshokutwa, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kiiza alifunga bao hilo, kwa kichwa akiunganisha krosi ya karibu ya Haruna Niyonzima ambaye alitumia mwanya wa mabeki wa APR kuzubaa wakisikilizia maamuzi ya refa, baada ya Kiiza kuangushwa.
Yanga waliinuka na wakaanzisha shambulizi la haraka lililozaa bao hilo. Dakika tatu baada ya bao hilo, beki wa Yanga, Godfrey Taita alitolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na sasa ataikosa fainali.
Ikumbukwe mwaka jana, Yanga iliifunga Simba SC katika fainali bao 1-0 na kutwaa taji la nne la michuano hiyo, baada ya awali kutwaa Kombe hilo 1975, 1993 na 1999.
Mapema katika Nusu Fainali ya Kwanza, Azam FC iliitoa AS Vita kwa kuifunga mabao 2-1, mabao yake yakifungwa na John Bocco ‘Adebayor’ na Mrisho Ngassa, wakati la Vita ya DRC lilifungwa na Mfongang Alfred.
Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul/Shamte Ally/Juma Seif, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Godfrey Taita, Haruna Niyonzoma, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na David Luhende.
APR; Jean Ndoli Claude, Olivier Karekezi, Suleiman Ndikumana, Mugiraneza Jean, Johnson Bogoole, Lonel St Preus, Ngabo Albert, Iranzi Jean Claude, Mbuyu Twite, Dan Wagaluka na Tuyizere Donatien.
 Mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza akimiliki mpira huku akizongwa na beki wa APR.

 Kipa wa APR, Ndoli Jean Claude akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake. Kusho ni mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza.

 Mfungaji wa bao pekee la Yanga, Hamisi Kiiza, akimtoka beki wa APR, Ngabo Albert katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Kagame, uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga imeshinda 1-


0. 
 Mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi akimtoka beki wa APR.

 Mashabiki wa Yanga.
 Wanazi wa Yanga wakishangilia ushindi wa timu yao.
 Wachezaji wa Yanga wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuingia fainali ya kombe la Kagame

 Kocha wa APR, Ernest Brandy (kushoto) akiwa na kocha wa Yanga, Tom Saintfiet kabla ya mchezo wa nusu fainali ya kagame ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

 Mrisho Ngasa akimtoka beki wa AS Vita
 Godfrey Taita akitafuta mbinu za kumtoka beki wa APR, Iranzi Jean Claude

 Kocha wa Yanga, Tom Saintfiet akikumbatiana na baadhi ya viongozi wa Yanga waliokuwa katika benchi la ufundi 

 Mshambuliaji wa Azam, Kipre Tchetche akimtoka beki wa AS Vita.
 Mashabiki wa Azam wakiishangilia timu yao baada ya kuingia fainali ya kagame

 Mshabiliaji wa Azam, Mrisho Ngasa akimtoka beki wa AS Vita, Pambani Makiadi katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ambapo Azam imeshinda kwa mabao 2-1 na kuingia fainali ya michuano ya kombe la Kagame kwa kupambana na Yanga Julai 28.

No comments:

Post a Comment