Thursday, July 26, 2012

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AKUTANA NA MABALOZI LEO

 

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,akizungumza na ujumbe wa Uongozi wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,ukiongozwa na Rais wa Jumuiya hiyo Awadh Ali Said,(wa pili kushoto).Picha na Ramadhan Othman,ORZ.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Kiongozi wa Mabalozi waliopo Tanzania,pia Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo JUma Alfani Mpango,(katikati) na Balozi wa Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu(UAE) pia Kiongozi wa Mabalozi wa Nchi za Kiarabu nchini Tanzania,Mallalla Mubarak  Suweid  El-Amri, walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa Mazungumzo. 
 Diwani wa Kata ya Kwadelo, Alhaji Omari Kariati (wa tatu kushoto) akiwa kwenye trekta na wakulima wa Kata hiyo, Abdallah Ramadhani (kushoto), Gabriel Galahenga, baada ya kuwakabidhi wakulima hao matrekta manne, kwenye Ofisi za Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)-SUMA JKT, Mwenge jijini Dar es Salaam, leo Julai 26, 2012. Kufuatia walikuma hao kukabidhiwa trekta hizo nne, sasa Kata hiyo ina trekta 20 zilizopatikana kutoka kampuni hiyo kwa udhamini wa diwani Kariati. Trekta moja  ambayo inauzwa kwa sh. milioni 20 wakulima hao wanakabidhiwa kwa kulipa nusu ya bei hiyo na kisha kulipa  zilizobaki katika kipindi cha miaka minne kwa udhamini wa diwani huyo.

Diwani wa Kata ya Kwadelo, Alhaji Omari Kariati, akimkabidhi funguo za trekta, mkulima wa Kata hiyo, Abdallah Ramadhani,  katika hafla ya diwani huyo kukabidhi matrekta manne wakulima kutoka kata hiyo, kwenye Ofisi za Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)-SUMA JKT, Mwenge jijini Dar es Salaam, leo Julai 26, 2012. Kufuatia walikuma hao kukabidhiwa trekta hizo nne, sasa Kata hiyo ina trekta 20 zilizopatikana kutoka kampuni hiyo kwa udhamini wa diwani Kariati. Trekta moja  ambayo inauzwa kwa sh. milioni 20 wakulima hao wanakabidhiwa kwa kulipa nusu ya bei hiyo na kisha kulipa  zilizobaki katika kipindi cha miaka minne kwa udhamini wa diwani huyo. Wengine, ni wakulima wa kata hiyo ya Kwadelo,  Alifa Hurufya, Gabriel Galahenga (wapili kushoto) na Meneja wa Mradi wa SUMA JKT, Kanali Felix  Samillan.
 

RAIS KIKWETE AKUTANA NA ASKOFU MKUU PROTASE RUGAMBWA, IKULU

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amekutana na kufanya mazungumzo na Askofu Mkuu Protase Rugambwa ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Baba Mtakatifu Benedict wa XVI kuwa Katibu Mwambata wa Idara au Kongregasio ya Uenezaji wa Injili kwaajili ya Mataifa na Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari yenye makao yake, Roma.

 
Wakati wa mazungumzo hayo Rais Kikwete kwa mara nyingine tena,amempongeza Askofu Rugambwa kwa uteuzi wake na kusema kuwa uteuzi huo ni kielelezo dhahiri cha imani kubwa aliyonayo Baba Mtakatifu kwa askofu huyo na kuwa ni heshima kubwa kwa mtanzania kupata nafasi ya kushika wadhifa huo mkubwa.Kabla ya Uteuzi huo Askofu mkuu Rugambwa alikuwa askofu wa jimbo Katoliki Kigoma (picha na Freddy Maro)

No comments:

Post a Comment