Sunday, August 5, 2012

CHADEMA WATIWA NGUVUNI LEO MJINI MOROGORO NA JESHI LA POLISI, SITA WAPELEKWA LUPANGO BAADA YA KUKUTWA NA MAGARI YAKUHAMASISHA MKUTANO NA MAANDAMANO.

 

Wafuasi wa Cha Cha CHADEMA wakiwa Chini ya Ulinzi wa Jeshi la Polisi baada yakutuhumiwa kuhamasisha mkutano haramu uliopigwa marufuku na Jeshi hilo. Wafuasi hao walikua na magari ya vipaza sauti wakihasisha watu kushiriki kwenye Mkutano huo leo mjini Morogoro.
WAFUASI  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Morogoro na magari yao wametiwa mbaroni kwa kosa la kufanya matangazo ya kuhamasisha wananchi kushiriki mkutano na maandamano ya chama hicho Jumamosi Agost 4 mwaka huu.
Kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na wafuasi hao wa Chadema kukiuka agizo la Kamanda wa Polisi mkoani humo Faustine Shilogile la kusitisha mikutanon na maandamano yaliyopangwa kufanywa na Chama hicho na Chama Cha Mapinduzi (CCM) hadi maonyesho ya nanenane yamalizike.

No comments:

Post a Comment