Jay'z ni mwanamuziki mwenye mafanikio makubwa sana, mafanikio yake yametokana na jinsi anavyoweza kujiingiza katika biahashara mbali mbali. Ukiachia musiki wake pia anabiashara zingine nyingi zinazo mwingizia pesa. Mimi na wewe hatuezi kuzijua zote lakini kuna hizi tatu musiki, nguo na sasa kuwa owner wa timu ya basketball inayojulikana New Jersey Nets akishirikia na tajiri mkubwa sana anaejulikana kwa jina la Mikhail D Prokhorov kutoka Russia na wameweza kuiamisha timu hiyo kutoka New Jersey hadi Brooklyn New York, na kuibadirisha jina baada ya kuitwa New Jersey Nets na sasa timu inajulikana kwa jina la Brooklyn Nets. Hapa chini ni picha ya sehemu ya uwanja maeneo ya downtown Brooklyn.
Picha hii ni uwanja huo ukiwa katika matengenezo ya mwisha hadi ifikapo september utakuwa umekamilika na utakuwa tayari kwa kutumiwa na michezo yake ya nyumbani ya timu hiyo ya Brooklyn Nets kama itakavyo julikana. Pita pita ya Vijimambo ilipata ukodak huu live katika eneo hilo la downtown Brooklyn maarufu kama Jay Street.
Picha hii ni Downtown Brooklyn, Ny
Uwanja utakavyo onekana baada ya kukamilika na unaweza kuona alama na namba husika za usafiri wa train au maarufu kwa jina la Subway, Train zitakazo pita hapa kama ukibahatika kutembelea New York na kutaka kwenda kuona uwanja huu unaeza kutumia train zenye alama hizo hapo juu. Gharama za ujenzi wa uwanja huu hadi unakamilika ni billion 1.
Sehemu ya kuchezea itakavyo onekana kwa ndani, New York sasa kutakuwa na timu mbili za basketball New York Knicks yenye kutumia uwanja wa nyumbani Madison Square Garden uwanja uliopo Midtown Manhattan na Brooklyn Nets uwanja utakuwa Downtown Brooklyn, NY.
Ukitaka kufika huo uwanjani wa Brooklyn Nets, Barcklays Center unaezakuendesha kwa kupitia daraja hili linaloitwa Broocklyn Bridge au hilo lingine la kushoto Manhattan Bridge kama unavyo ona, picha na NY Ebra, Vijimambo New York City.
No comments:
Post a Comment