Wednesday, August 29, 2012

UKISTAAJABU YA MUSSA....NI KWELI YAMETOKEA KIJANA AFUNGA NDOA NA MAMA YAKE MZAZI BAADA YA BABA YAKE KUFARIKI


Mke na Mume, Bi Condorada Ngonyani (70) na Bw. Joseph Mapunda, ambao ni Mama na Mwanawe, wakiwa nje ya nyumba ya Mganga, wakati walipofikishwa kwa suala hilo la Mama Mzazi na Mwanawe kufunga ndoa.
Na Mwandishi Wetu, Namtumbo Ruvuma
MARA kadhaa kumekuwa kukijitokeza matukio mbalimbali ya kustaajabisha, kusikitisha na kutisha na mengine yakihisiwa kuwa ni imani za kishirikina, ambapo mengi ya matukio hayo ambayo hutokea si kwingine ni hapa hapa nchini kwetu, huwaacha watu hoi na maswali mengi yasiyokuwa na majibu.
Kwa mara nyingine tena tukio la kushangaza na kutoaminika kama ni kweli ambalo huwezi hisi kuwa ni la imani za kishirikina, kwani wahusika wote wamefanya hivyo kwa malengo na kuweka wazi sababu za kufanya hivyo japo si sahihi kwa itikadi za kidini, mila na destuli za mtanzania
Tukio hili ni Mama Condorada Ngonyani (70) mkazi wa mkoani Ruvuma, ambaye aliamua kufunga ndoa na mtoto wake wa tatu wa kiume wa kimzaa na kuishi naye kinyumba kama mke na mume, ambapo wameonekana wao kama wao kuwa wapo sahihi na kuwashangaa wanadam, majirani zao na Jamii kwa ujumla kuingilia mapenzi yao.
Wananchi wapatao 400, wa mkoa wa Ruvuma walijitokeza kushuhudia kimbwanga hii wakati uongozi wa Serikali ya Mtaa walipoamua kuwafuatilia na kuwahoji na kuitisha mkutano wa wanakijiji na kuwaweka hadharani, ambapo Wananchi wa Mkoa wa huo wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maendelo ya Jamii, Jinsia na watoto, kufuatilia kwa karibu suala hilo na kuwaondoa hofu wananchi kama kuna sheria inayomruhusu Mtoto na Mama Mzazi kuweza kuishi kindoa.
Alipohojiwa Mama huyo, Condorada Ngonyani, anasealisema kuwa mara tu baada ya kufariki mume wake, Mzee Mapunda, yeye aliamua kumchagua mtoto wake huyo Joseph Mapunda, ili amrithi baba yake katika kuumiliki mwili wake kama ambavyo alikuwa akifanya Baba yake mzazi, ili kuondokana na tamaa na vishawishi wa kiulimwengu.
Alisema kuwa baada ya uteuzi huo walifunga ndoa ya kimila japo kuna baadhi ya wanafamilia hawakufurahishwa na tukio ama jambo hilo, lakini yeye aliamua kufunga masikio na kuamua kuvunja amri ya sita na mtoto wake huyo wa kumzaa.
Tukio kama hili ni mara ya kwanza kutokea kwa mkoa wa Ruvuma na hata kwa Tanzania nzima, ambapo wakaazi wa Ruvuma wamekuwa wakibaki na maswali mengi juu ya tukio hilo na kuhoji Jamii sasa inaelekea wapi kwa baadhi ya Watanzania kuibomoa wenyewe mila na desturi zetu.
Kwa upande wake, Joseph Mapunda, yeye anasema kuwa upendo na mahaba anayoyapata kutoka kwa mkewe huyo ambaye ni mama yake mzazi, hajawahi kuyapata kokote na kusema kuwa wanapendana sana na wanaheshimiana kama mke na mume.
Josepha amehiji kulikoni wanadam kuwafuatilia katika mapenzi yao na kusema kuwa ''hawa watu wanaotufuatilia hadi leo hii kutuweka hadharani namna hii, wanataka nini kwetu?''.
Wananchi hao waliofurika kwa Mganga wa Jadi Flora Ndembo, wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma, wameiomba Serikali kuingilia kati suala hilo na kuchukua hatua kisheria ili iwe fundisho kwa wanatanzani wengine wenye akili kama hizo za kuharibu mila na desturi za kitanzania kirahisi kama hivyo. Picha na Songea Habari


Bi. Condorada Ngonyani. ''Nawashangaa wanadam kuingilia mapenzi yangu, mtuache''.
 
 


Bwana, Joseph Mapunda, ''Wananchi mtatutakia nini na mapenzi yetu???

No comments:

Post a Comment