Saturday, August 4, 2012

WALIMU WAREJEA KAZINI BAADA YA MAHAKAMA KUTOA HUKUMU

 

Rais wa Chama cha Walimu Tanzania CWT, Gratian Mukoba.

Chama Cha Walimu Tanzania-CWT-kimetangaza kusitisha rasmi mgomo wa walimu na hivyo kuwataka walimu wote nchini kurejea kazini mara moja kuanzia leo ili kutekeleza majukumu yao ya kila siku kama kawaida.
Akitoa tamko la CWT kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, baada ya Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi kukiagiza Chama hicho kitoe maelekezo kwa wanachama wake kurudi kazini, Rais wa Chama hicho, Gratian Mukoba,  amesema walimu wanarudi kazini huku wakiwa wamekata tamaa kutokana na hukumu hiyo.
Aidha Mukoba, amefafanua kuwa walimu wanaporudi kazini bila kuwa na mawazo yaliyotulia, utendaji wao utaathirika kwa namna moja au nyingine, hivyo Chama kinatoa wito kwa Serikali kukutana na CWT kwa haraka ili kuendeleza majadiliano ya Madai mapya ya Walimu.
Kuhusu kulipa fidia ya hasara waliyoipata wanafunzi, iliyotolewa na Mahakama, Chama hicho kimesema kinasubiri taarifa rasmi ya Serikali kuhusu hasara hiyo kwa kuwa hakina uwezo wa kufahamu hasara waliyoipata wanafunzi nchini nzima.
Kwa mujibu wa Mwalimu Mukoba, wenye uwezo wa kuwasilisha hasara hiyo ni mlalamikaji katika kesi hiyo ambaye ni Serikali.
Hapo jana Chama hicho kilipongeza kauli ya Rais Jakaya Kikwete,  aliyoitoa kwa kusema Serikali inajali na kuthamini mchango wa Walimu nchini.

FLOYD MAYWEATHER ATOKA JELA

Bondia machachari, Floyd Maywether,  akiwa na

furaha baada ya kuwaona mashabiki wake wakiwa

 nje ya Lango la Gereza hilo baada ya kutoka nje.

  Bondia huyo amechiwa huru jana asubuhi baada ya

 kutumikia kifungo chake cha miezi miwili

 alichohukumiwa kwa kumdhalilisha rafiki yake wa

 kike mbele mtoto wake.

Akipokelewa na ndugu na jamaa zake baada ya


kutoka nje.
Akiagana  na mashabiki wake na kuingia garini kuelekea nyumbani.

No comments:

Post a Comment