Monday, September 10, 2012

HAPPINESS MAGESE ATISHA MITINDO MAREKANI, AKINA BECKHAM WAHUDHURIA KUMUONA, ALIYEMVALISHA MKE WA OBAMA NAYE NDANI

Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Happines Millen Magese akishiriki Wiki ya Mitindo ya Mavazi ya New York nchini Marekani jana. Onyesho hilo lilishuhudiwa na nyota wakubwa kama mwanasoka David Beckham huku wabunifu wakubwa duniani wakishiriki kuonyesha mitindo yao ya mavazi kama Tommy Hilfiger, Carolina Herrera, Michael Kors, Ralph Lauren na mwanamama Tracy Reese, ambaye gauni lake lilivaliwa na mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama katika Kongamano la Kitaifa Chama cha Democratic. Mwanamitindo maarufu Naomi Campbell pia alipita stejini kuonyesha mitindo. Picha: REUTERS
Nyota wa soka David Beckham (kulia) akisimama mbele ya muimbaji Natasha Bedingfield (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Adidas, Erich Stamminger (wa pili kulia) kabla ya kuanza kwa onyesho la mavazi katika Wiki ya Mitindo ya New York ya Y-3 Spring/Summer 2013 collection jana Septemba 9, 2012. Picha: REUTERS
Mbunifu wa mitindo ya mvazi Zac Posen (katikati) akipita stejini na wanamitindo Naomi Campbell (kushoto) na Coco Rocha (kulia) baada ya kuwasilisha mitindo yake ya mavazi ya majira ya joto 2013 wakati wa Wiki ya Mitindo ya New York jana Septemba 9, 2012. Picha: REUTERS
Mbunifu wa mitindo ya mavazi Tommy Hilfiger akipungia waliohudhuria baada ya kuwasilisha ubunifu wake wa mitindo ya mavazi ya majira ya joto 2013 wakati wa Wiki ya Mitindo ya New York jana Septemba 9, 2012. Picha: REUTERS
Muimbaji Natasha Bedingfield (katikati) akipozi kabla ya kuanza onyesho la mavazi katika Wiki ya Mitindo ya New York ya Y-3 Spring/Summer 2013 collection jana Septemba 9, 2012. Picha: REUTERS
Mimi ndo nambunia mavazi mke wa Obama.... Mbunifu wa mitindo ya mavazi Tracy Reese akiishukuru hadhira baada ya kuwasilisha ubunifu wake wake wa mitindo ya mavazi ya majira ya joto 2013 wakati wa Wiki ya Mitindo ya New York jana Septemba 9, 2012. Tracy Reese amekuwa akimbunia mavazi Michelle Obama likiwamo alilolivaa katika Kongamano la Kitaifa Chama cha Democratic.Picha: REUTERS

Mwanamitindo akipita kuonyesha mavazi wakati wa Wiki ya Mitindo ya New York jana.

Mwanamitindo akipita kuonyesha mavazi wakati wa Wiki ya Mitindo ya New York jana.
Mwanamitindo akipita kuonyesha mavazi wakati wa Wiki ya Mitindo ya New York jana.

Nyota wa soka David Beckham (kulia) akikaa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Adidas, Erich Stamminger (katikati) kabla ya kuanza kwa onyesho la mavazi katika Wiki ya Mitindo ya New York ya Y-3 Spring/Summer 2013 collection jana Septemba 9, 2012. Picha: REUTERS

Nyota wa soka David Beckham (kulia) akikaa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Adidas, Erich Stamminger kabla ya kuanza kwa onyesho la mavazi katika Wiki ya Mitindo ya New York ya Y-3 Spring/Summer 2013 collection jana Septemba 9, 2012. Picha: REUTERS

Wanamitindo wakijiandaa nyuma ya steji kwa ajili ya onyesho la mavazi katika Wiki ya Mitindo ya New York ya Y-3 Spring/Summer 2013 collection jana Septemba 9, 2012. Picha: REUTERS
Wanamitindo wakipita stejini wakati wa onyesho la mavazi katika Wiki ya Mitindo ya New York ya Y-3 Spring/Summer 2013 collection jana Septemba 9, 2012. Picha: REUTERS

Wanamitindo wakipita mbele ya hadhira wakati wa onyesho Wiki ya Mavazi ya New York