Mama Salma Kikwete akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Mwanaidi Sinare Maajar, Balozi wa Umoja wa Afrika katika Umoja wa Mataifa Mhe. Amina Salum Ali na Mshauri wa Rais mambo ya Diplomasia Balozi Liberata Mulamula kabla ya kuhudhuria mkutano wa African First Ladies Roundtable jijini New York, Marekani, leo
Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Bibi Katalin Bogyay Balozi wa Hungary UNESCO na amebobea katika diplomasia ya utamaduni na mtetezi mkubwa wa masuala yahusuyo fursa sawa ya elimu kwa mtoto wa kike.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo
Mama Salma Kikwete akihudhuria mkutano huo
Baadhi ya washiriki
Mama Salma Kikwete akipokea vipeperushi katika mkutano huo
Mama Kikwete akisalimiana na baadhi ya washiriki
Picha ya pamoja
SIMU ZA MKONONI ZINAWEZA KUWAKOMBOA
WANAWAKE KIUCHUMI - SALMA KIKWETE
Na Mwandishi Maalum
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete , amesema tekinolojia ya mawasiliano ya simu za mkononi, kama ikitumiwa vema, inaweza kuwa chombo muhimu katika kuchagiza na kuwaletea maendeleo ya haraka wanawake na wasichana hususani wale wa vijijini.
Mama Kikwete ameyasema hayo, wakati alipokuwa akitoa mchango wake katika majadiliano ya kwanza na ya aina yake. Majadiliano yaliyowaleta meza moja, baadhi ya wake wa marais, wakurugenzi wa makampuni,wahadhiri na wanadiplomasia, kujadiliana na kubadilishana mawazo na mbinu zitakazoweza kuwahamasisha watoto wa kike kuchangamkia masomo ya Sayansi, Tekinolojia, Uhadinsi na Hesabu ( STEM)
Majadiliano hayo ambayo yalifunguliwa na Bi. Anitta Kalinde, Waziri wa Masuala ya Jinsia kutoka Malawi kwa niaba ya Rais wa Malawi.Yamefanyika siku ya jumatatu katika ukumbi wa mikutano wa jengo la Credit Suisse, Jijini New York.
Aidha Majadiliano hayo , yalilenga pia kuwachagiza viongozi hao kutumia nafasi walizo nazo, uelewa wao na uwezo walionao katika kuwasaidia wanafunzi wa kike kung’amua mapema vipaji vyao na hivyo kupata fursa ya kuvitumia vipaji hivyo kufikia malengo, matarajio na ndoto zao kuhusu maisha yao ya baadaye.
Kupitia teknolojia ya simu za mkononi, Mama Salma amebainisha kwamba kwa nchi za Afrika ikiwao Tanzania, siyo tu kwamba ni tekinolojia rahisi ya mawasiliano lakini inawawezesha wanawake, kubuni na kuanzisha miradi ya kiuchumi kwa kuwa mawasiliano hayo yanawapa fursha ya kupata habari na kubadilishana mawazo na makundi mbalimbali ya jamii.
“ Ninawashukuru kwa kunialika katika majadiliano haya, lakini kilichonifurahisha zaidi ni mada yenyewe. Tunahitaji kukusanya nguvu zetu, uwezo wetu na maarifa yetu kuwasaidia wanawake na wasichana wa vijijini kunufaika na tekinolojia rahisi zilizopo kujiletea maendeleo yao na kuondokana na umaskini”. Akasema Mama Salma
Na kuongeza, tekinolijia hiyo ya simu za mkononi ni mfano mmoja tu lakini zipo teknolojia nyingi na rahisi ambazo kwazo zinaweza kuwanufaisha wanawake na wasichana ikiwa watapewa na kuwezeshwa kujifunza masomo ya sayansi, hesabu, uhandisi na tekinolijia.
Na kwa sababu hiyo, Mke wa Rais amesema, ili wanawake na wasichana wanaweze kunufaika na teknolijia zilizopo kunahitajika ushirikiano na ubadilishanaji wa mawazo na uzoefu wa namna bora ya kuwasaidia.
“Wito wangu kwetu sote tuliokusanyika hapa, ni huu, tujenge mitandao, tubadilishane uzoefu, na utaalamu wa kuwasaidia wanawake na watoto wa kike na kwa upande mwingine kuwapa fursa wanawake na wasichana nao kutembeleana na kujufunza baina yao”. Akasisitiza.
Aidha amesema kwa kutambua umuhimu wa wasichana kupata elimu, ikiwamo maarifa na ujuzi mbalimbali. Yeye binafsi kupitia taasisi yake ya wanawake na Maendeleo ( WAMA) imekuwa mstari katika kuwasaidia watoto wa kike kufikia malengo yao.
Akatumia nafasi hiyo, kuwakaribisha wajumbe wenzie kutembelea Tanzania na kujionea jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali na WAMA katika kusukuma mbele maendeleo ya wanawake na watoto wa kike.
Katika maajadiliano hayo, baadhi ya washiriki akiwamo Bibi Savanna Maziya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Makapuni ya Bunengi ( Bunengi Group of Companies), na mwanzilishi wa majadiliano hayo, wameonyesha nia ya kuja Tanzania kutambua maeneo ya ushirikiano hususani katika eneo hilo la kuwasaidia na kuwawezesha watoto wa kike kumudu masomo ya STEM.
Tayari Bibi Savanna kupitia Kampuni yake ameanza kuwasaidia wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu kumudu na kuyakabili masomo ya sayansi katika baadhi ya shule nchini Marekani, na tayari ameanza kuona mafaniko makubwa kwa watoto hao kufanya vizuri
Aidha Dkt, Herta von Stiegel, Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa Kampuni ya Ariya Capital Group Limited yeyé, na ambaye tayari kampuzi yake imeanza kuwekeza nchini Tanzania katika uvunaji wa umeme wa upepo. Anasema kwa kadri hali ya mabadiliko ya dunia yanavyoendelea, Afrika inabaki kuwa ndilo bara lenye raslimali nyingi zikiwamo za ardhi, madini na nguvu kazi kubwa.
Akasema wakati idadi ya watu ikipungua katika nchi zilizoendelea, idadi ya watu inaongezeka barani afrika na kwa sababu hiyo akashauri kwamba idadi ya watu inayoongezeka barani afrika inapaswa kutumika si tu kama nguvu kazi, bali yenyewe iwezeshwe ili ichukue nafasi ya kuendesha uchumi na maendeleo ya nchi zao.
Dkt. Stiegel amesema huu ni wakati muafaka pia kwa makapuni ya kibiashara kutafuta fursa za uwekezaji nchini Tanzania, nchi ambayo ameitaka kama yenye vivutio vingi vya uwekezaji.
No comments:
Post a Comment