Tuesday, September 11, 2012

Mapenzi siyo presha, ila presha inaletwa na mpenzi uliyenaye

ANAWEZA kuwa nawe kwa sababu anavuta muda au anasubiri mambo yake yamnyookee akuache solemba. Inawezekana kweli akawa anakupenda lakini tabu ya mabrazameni na masistaduu mapenzi yao huwa nusunusu. Hata siku moja huwa hayakamiliki. Mifano ipo mingi ndiyo maana najenga hoja hii.
Yule brazameni ambaye alikuwa anajifanya anampenda mrembo wa umri wake, maisha yakawa matamu na kila mtu akadhani watafika mbali lakini baadaye yakatokea ya kutokea, kijana akaangukia kwa jimama anayejua kulea, matokeo yake bila huruma, akampiga teke mpenzi wake akiwa hajui la kufanya.
Siku zote unapowekeza upendo wako kwa brazameni au sistaduu, unapaswa kuwa mwangalifu, vinginevyo unaweza kujaa machozi mengi. Wewe kijana wa kiume, mpende na kumjali mwenzi wako lakini siku akipata mtu anayedhani ana fedha kuliko wewe, atamkimbilia na kukuacha na mateso ya moyo.
WANAPENDA KULELEWA
Hili ni jibu la yale ambayo nimeyaeleza kwenye kipengele kilicho hapo juu (Mtego wa Fedha). Unaweza kujiuliza ni kwa nini masistaduu na mabrazameni ni watumwa wa fedha. Jawabu ni kwamba wanapenda sana kulelewa ndiyo maana wanakuwa wepesi kushawishika na kukimbilia kwa wenye uwezo kifedha.
Asili yao ni watu magoigoi kwenye utafutaji. Hupenda kujilegeza, yaani wao ni lainilaini. Hali hiyo ndiyo huwafanya kuwa watumwa wa watu ambao hata hawawapendi. Kibinti kidogo kutembea na mzee mfano wa babu yake au kijana kujitumbukiza kwenye penzi la ajuza, anayemzidi umri hata mama yake mzazi.
Hii ikupe sababu ya kuona hatari iliyo mbele yako pale utakapojielekeza kwa mwenzi wako ambaye ana asili ya wale ambao nimewataja hapo. Fikiria kwamba wanataka muda wote wawe wamependeza hata kama hawana fedha, je, watakubaliana na maisha yako ya upendo wakati wanaona kuna sehemu ya fedha?
NIMALIZE KWA MFANO
Kuna ndugu yangu mmoja anaitwa Ponda, huyu ni mwanajeshi wa JWTZ, kutokana na sifa yake kitaaluma, aliwahi kuwa mwalimu Shule ya Sekondari Makongo. Huyu alikuwa na mke wake ambaye ni mtumishi wa Jeshi la Magereza. Tatizo la ndugu yangu huyo likawa ni kudanganywa na muonekano wa masistaduu.
Akiwa anafundisha, akadondokea kwa mwanafunzi wake ambaye ni sistaduu wa kutupwa. Baada ya kukolea kwa mwanafunzi huyo, akaanza kumletea visa mkewe (askari magereza). Zaidi akawa anamsimanga kuwa hajasoma na kwamba alikosea kumuoa. Mama ikamuuma, mwisho akaamua kuomba talaka.
Baada ya kuachana, Ponda akasubiri huyo sistaduu amalize kidato cha nne halafu akafunga naye ndoa. Unadhani maisha yalikuwa mazuri? Haikupita miezi mingi, ndugu yangu huyo akaanza kuona machungu ya kuoa mwanamke wa sampuli hiyo. Aliteseka kupita maelezo.
Mke sistaduu huyo alianza kutoa penzi hovyo kwa kila aliyemuona ananukia fedha. Akaja kugundua kuwa mke wake ni kiwembe, kwani huwatongoza hata ndugu zake kisa tu apate fedha. Ponda akaumia, akawa anagombana na ndugu zake. Makosa ya mkewe lakini hakuyaona. Kipendacho roho hula nyama mbichi.
Siku moja Ponda akasoma SMS ya mkewe kwenda kwa mtoto wa dada yake. Hiyo iliandikwa: “Samahani Anko, nina shida ya shilingi 500,000 mtu atakayenipa, naweza kumpa hata penzi. Hata kama ni wewe nitakupa, sitajali kama wewe ni mjomba wa mume wangu. Sijali kabisa, nataka fedha.”
Ponda kuona hiyo SMS akagombana na huyo mtoto wa dada yake. Kwani walifika mbali basi? Leo hii sistaduu huyo ni mke wa mganga mmoja wa dawa za asili, kwani alipoona huyo mganga ana fedha kuliko mumewe, alimkimbilia kwa tamaa zake. Ponda ni kilio. Usiombe kukutana na masistaduu au mabrazameni, wana mambo ya ajabu, watakutesa. Kuwa makini siku zote.

No comments:

Post a Comment