Tuesday, September 4, 2012

SERIKALI, SUMATRA, ABIRIA TUSISUBIRI YATOKEE CHUKUA HATUA SASA, KINGA NI BORA KULIKO TIBA



 Pamoja na matukio kadhaa ya ajali za meli na Boti, na agizo lililotolewa nanSumatra na Serikali kwa ujumla wa kutopakia abiria kuzidi uwezo wa Chombo husika, lakini bado si abiria wala wahusika wanaotilia mkazo suala hili na kufuata sheria na taratibu hadi likitokea tatizo jingine kila mtu ataanza kusema juavyo na wengine kutoa lawama kwa Serikali.
 Kwa upande mmoja ama mwingine unaweza kuilaumu Serikali kwa kutosimamia iapasavyo taratibu ilizoweka kuhusiana na suala hili kwani hadi kufikia chombo kukata tiketi zilizozidi idadi ya Siti zake wakati wasimamizi wapo tunashindwa kupata majibu yaliyo sahihi kwamba wapo kazini ama wanakuwepo pindi tu yanapotokea matatizo??, na kama wapo kweli je wamelala na kucheza gem za Karata katika Kompyuta zao au na wao wanachao katika hili? yaani huenda zikizidishwa tiketi na chombo kikaondoka salama basi chochote kitu kitarudi kwa jamaa wa zamu?. 
Hebu angalia pichani juu abiria kibao wakiwa wameachwa chini na chombo hiki cha Express kikiondoka na kuwaacha kuelekea Bara huku wakiwa na tiketi zao mikononi.
 Na hapa ni ndani ya Boti hiyo abiria kibao tu wakiwa wamesimama kwa kukosa siti ambazo zimejaa kuanzia chini hadi juu, ambapo kila mmoja hapa ana tiketi yake mkononi.
 Abiria wakiwa wamekaa juu ya mashine za Boti hiyo ndani wakati ikiendelea na safari yaa kuelekea Bara baada ya kukosa Siti.
Na wengine wakisimama nyuma kama hivi si kwa kupunga upepo ama kufuata jua, la hasha bali wamelazimika kusimama eneo hili baada ya kukosa siti, na ikumbukwe na wengine waliachwa chini pale Bandarini Zanzibar, sasa cha kujiuliza ni kwamba je inamaana mpaka sasa bado tiketi zinaendelea kuuzwa kimagumashi mikononi  nje ya ofisi husika ama ni mazoea ndiyo yanachukua nafasi yake?

No comments:

Post a Comment