Tuesday, October 2, 2012

EAC PHOTO WAANZA KUNASA PICHA ZA KUMBUKUMBU KISIWANI ZANZIBAR



JUMUIA ya Nchi za Afrika Mashariki (EAC) ipo katika mpango maalum wa uboreshaji wa Maktaba ya Picha za kumbukumbu ya Matukio ya Kihistoria na vitu mbalimbali vinavyohusiana na Umoja huo kwa nchi zote wanachama.
Kazi ya Upigaji picha hizo inafannywa na Wapiga picha bora kumi kutoka jumuia hiyo ambao baada ya kupatikana walipatiwa Mafunzo maalum ya upigaji Picha na Utengamano wa Jumuia ya Afrika Mashariki , mafunzo yaliyofanyika jijini Arusha chini ya Shirika la Kijerumani la GIZ.
Zoezi la upigaji picha hizo zilizokatika ubora wa hali ya juu ulianza juma lililopita Nchini Kenya na sasa timu ya Wapigapicha hao wapo Nchini Tanzania na wameanzia katika Kisiwa cha Zanzibar ambacho kipekee katika mambo muhimu ya EAC kina mambo mengi ya Kihistoria.
Pichani ni Kundi la Wapiga picha hao Mroki Mroki (katikati), Filbert Rweymamu (kushoto) wakiongozwa na Mtaalam Harmut Fiebig (wapili kulia) kutoka nchini Ujerumani ambaye anafanyia Shughuli zake nchini Kenya. Wengine katika picha hiyo ni Mpigapicha wa Kujitegemea Zanzibar Martin Kabemba kulia na Ofisa Kutoka Kitengo cha Habari EAC, Sk Chhatbar.
Bendera ya EAC ikipepea katika Jahazi Kisiwani Zanzibar
Wakionesha Mtangamano kwa kugonganisha vikombe vyao vya Kahawa
Misikiti ya kale


Majengo ya Kale ya Kihistoria ni moja ya picha zitakazo hifadhiwa katika Maktaba hiyo ya Picha ya Jumuia ya Afrika Mashariki, na Endapo Wanahabari, na watafiti watahitaji kuzitumia basi zitapatikana kwa urahisi.
Mahabusi ya Watumwa Zanzibar
Sanamu za Watumwa

No comments:

Post a Comment