Friday, October 19, 2012

WAISLAMU WATEKELEZA HADHIMA YAO YA KUFIKA IKULU, SITA WAKAMATWA



Nje ya Ikulu kunavyo onekana kwa sasa
Huyu jamaa alipokamatwa alikuwa akisema "atakufa kwa jina la Allah" WALA SI MWINGINE NA ALISISITIZA HILO MUDA WOTE NA HAKIKA ALIKUWA ANAINGIA KWELI IKULU MAANA ALIFIKA MPAKA ENEO LA BUSTANI YA IKULU.
Baadhi ya waumini wanaodaiwa kutoka kikundi cha dini ya kiislamu wakiwa ndani ya gari la polisi baada ya kudhibitiwa eneo la jirani na geti la Ikulu, mapema leo ambapo jumla ya watu 6, walikamatwa.
WATU sita waliokuwa na nia ya kuandamana hadi Ikulu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi.
Watu hao waliokuwa wakifika katika viunga vya Ikulu mmoja mmoja kwa nia ya kuonana na Rais Jakaya Kikwete.
Hata hivyo jitihada zao hizo ziligonga mwamba baada kukutana na askari wa kutuliza ghasia.
Mmoja wa watu hao waliokamatwa aliwaeleza askari waliomkamata kuwa “Hata nikifa nitakwenda peponi naombeni mnipige na mniue maana na ninamshuhudia alah ,siogopi kabisa lakini lazima nionane na Rais” ni sauti ya mtu mmoja aliyekamatwa.
Msafara wa Rais Jakaya Kkwete uliofika Ikulu majira ya saa 7:48 ulishuhudia ulinzi mkali huku mmoja wa wafuasi hao akiwa anashikiliwa na polisi.
Watu hao pia walikuwa na chupa za maji,miswaki na sabuni ndani ya kanzu zao wakionekana kuwa tayari kwa lolote.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadiki, amepiga marufuku mihadhara yote ya dini mpaka hali ya usalama itakaporejea.
Aidha amezitaka Mamlaka zote zinazoshughulika na utoaji vibali vya mihadhara hiyo kuacha kufanya hivyo.
Akizungumza jana katika mkutano uliowajumuisha Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu(TEC),Padri Anthony Makunde.
Kwa upande wa Kova amekanusha taarifa iliyotolewa na badhi ya vyombo vya habari kuwa Jeshi hilo limewataka waislamu wote wa kikundi hicho na waislamu wote kujisalimisha kwa Jeshi hilo.
Kova alisema kuwa watu wanaotakiwa kujisalimisha kwa Jeshi hilo ni sita na kuwataja kuwa ni Mukadam Saleh Kondo, Saleh Juma Bungo,Shaaban Mapeo, Jaafar Mneki,Rajab Katimba na Amani Moshi.
Naye Padre Makunde alitoa rai kwa Watanzania kuendelea kuvumilia na kudumisha upendo na mshikamano uliopo miaka mimgi baina yao na kusema kuwa njia pekee ya kufikia suluhu ni mazungumzo bila jazba na hasira.
Naye Alhad Musa aliwataka waislamu,maimamu na masheikh kuwa na subira na kuepuka vitendo vya uvunjifu wa amani na kutojidanganya kuwa na jihad kwani haiji kwa uvunjifu wa sheria na kwamba nidhamu ya dini hiyo na utaratibu wake unakataa vitendo hivyo.

No comments:

Post a Comment