Friday, October 5, 2012

WAKENYA WATATU WASHINDA KUENDELEA NA RUFANI YA KESI ZA KUTESWA ENZI ZA UKOLONI.
Raia watatu wa Kenya sasa wanaweza kuendelea na utaratibu wa kuwasilisha madai yao ya kisheria ya kuteswana mamlaka za Uingereza kipindi cha ukoloni.

Jaji wa mahakama Kuu ya jijini London ametoa uamuzi huo unaohusiana na kesi ya maasi ya kundi la Mau Mau mnamo miaka ya 1950 japokuwa umeshapita muda mrefu.

Maelfu ya watu waliuawa wakati wa mapingamizi ya Mau Mau dhidi ya utawala wa Kiingereza nchini Kenya kipindi cha kati ya miaka ya 1950 na 1060.