Monday, December 31, 2012

UNIQUE MODEL 2012 MOTO WA KUOTEA MBALI




Unique model 2012 ya event kubwa za mitindo nchi
ni Tanzania,hapa mwanamitindo Zeenath akionyesha uwezo wa miondoko ya kimaonyesho ya nguo.
Unique models wakionyesha uwezo wa kudansi jukwaani.

Mambo yalikuwa hivi wadau.
Majaji wakifanya yao.
Mshindi namba tatu Amina Ayoub akiwapungia watu mkono baada ya ktangazwa.

Hali ilikuwa namna hii wadau.
Majaji wakitangaza matokeo.

Elizabeth Pertty Unique model-Talent 2012 akipungia watu baada ya kutangazwa.

Mwanamitindo akionyesha kipaji cha kuigiza kwa kutoa ujumbe kuhusiana na gonjwa la ukimwi.

Unique model of the year 2012 Catherine Masumbigama akipungia mkono mashabiki baada ya kutangzwa kuwa ndiye mwanmitindo wa mwaka 2012-2013.
Catherine akiwa na Balozi wa shindano la unique model Roseminner.
Grand finale.
 
Top five ni Zeeenath Ayoub,Cecilia Emmanuel,Elizabeth Pertty,Catherine Masumbigana na Amina Ayoub.

Alex Msama Atoa Misaada Kwa Watoto Yatima


Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa, Halima Ramadhani akizungumza waandishi wa habari kuhusu historia ya kituo chake baada ya kupokea misaada ya vyakula kutoka kwa kampuni ya MsamaPromotion ambapo mkurugenzi wake Alex Msama amekabidhi misaada hiyo leo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa, Halima Ramadhani. Mbali ya kukabidhi vyakula hivyo, Msama pia alikabidhi hundi ya sh milioni 1.5 kwa ajili ya kulipia ada za wanafunzi waliofukuzwa shule. Msaada huo umetokana na mapato ya tamasha la Pasaka, hafla hiyo ilifanyika Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula 
Baadhi ya watoto wakishusha vyakula viliyotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama
Baadhi ya watoto wakishusha vyakula viliyotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama
Baadhi ya watoto wakishusha vyakula viliyotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama
Baadhi ya watoto wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akimkabidhi hundi ya sh. milioni 1.5 Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa, Halima Ramadhani kwa ajili ya kulipia ada za wanafunzi waliofukuzwa shule. Mbali ya kukabidhi hundi, Msama alikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali vikiwa na thamani ya sh milioni 3 zilizotokana na mapato ya tamasha la Pasaka, hafla hiyo ilifanyika Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa, Halima Ramadhani akimuonesha moja ya vyumba vinavyotumiwa na watoto hao.
Alex Msama akipata maelezo katika chumba maalum kwa ajili ya watoto kujifunza

Askari Aliyepiga Picha Na Lema Atokomea



Na : Nuzulack Dausen

JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema askari anayedaiwa kuwa jeshi hilo aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ametoroka.

Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alisema jana kwamba pamoja na hatua yake ya kutoroka, jeshi litaendelea kumsaka kwa udi na uvumba ili kumhoji na kujiridhisha kama kweli ni mwanajeshi wake kabla ya kumchukulia hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Kifungu cha 147 cha Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya 1977.

“Huyu kijana inasemekana alishawahi kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), lakini wakati tunaendelea na uchunguzi alitoroka katika nyumba aliyokuwa amepanga bila ya taarifa kwa baba mwenye nyumba,” alisema Kanali Mgawe na kuongeza:

“Askari huyo alikuwa anaishi katika nyumba ya kupanga mita chache karibu na Kituo cha Polisi cha Simanjiro, Arusha na alikuwa akijishirikisha na ulinzi shirikishi.”

Alipoulizwa jina la askari huyo, Kanali Mgawe alijibu: “Yeye alikuwa anafahamika mtaani hapo kwa jina la kamanda.”

Hata hivyo, Kanali Mgawe alisema jeshi hilo litahakikisha linatoa ripoti kamili kwa umma baada ya kumkamata na uchunguzi kukamilika ili kuondoa utata uliogubika suala hilo.

Alipoulizwa kama kuna tofauti gani kati ya mwanajeshi kuingia kwenye mikutano ya wanasiasa na wale wanaofanya kazi za kisiasa kama wakuu wa wilaya na mikoa, Kanali Mgawe alijibu:” Wanajeshi wanaofanya kazi za U-DC au RC, wanaruhusiwa kisheria.”

Alifafanua kuwa iwapo mwanajeshi atateuliwa kufanya kazi katika taasisi yeyote ya Serikali nje ya jeshi, atatakiwa kuvua magwanda ya jeshi na kufanya kazi hiyo mpaka atakapomaliza muda wake na baada ya hapo ataruhusiwa kurejea jeshini.

“Kuna kitu kinaitwa ‘secondment.’ Mwanajeshi anaruhusiwa kufanya shughuli zozote nje ya jeshi iwapo atahitajika kufanya hivyo. Ila kwa masharti ya kuvua magwanda, hivyo wananchi wasishangae kuwaona baadhi ya askari wetu ni wakuu wa wilaya na mikoa na baadaye kurudi jeshini kuendelea na majukumu yao,” alisema Kanali Mgawe na kuongeza:

“Askari akiwa katika majukumu yake mapya, atafanya kazi zote atakazopewa zikiwamo za kisiasa kama ilivyo kwa wakuu wa wilaya na mikoa, lakini akirudi jeshini, anarudi kuwa askari mwenye utii na kufuata kanuni za jeshi zisizofungamana na siasa.”

ONYESHO LA BENDI YA AKUDO IMPACT MSASANI BEACH

Wanenguaji wa bendi ya Akudo Impact, wakishambulia jukwaa wakati wa onyesho lao, lililofanyika jana jumapili kwenye Ukumbi wa Msasani Beach Club, ambapo bendi hiyo hufanya onyesho la Bonanza katika ukumbi huo kila siku ya Jumapili.
Mashambulizi yanaendelea jukwaani,,,
Rapa wa bendi hiyo (kulia) akiwachezesha wanenguaji wa bendi hiyo wakati wa onyesha hilo.

RAIS WA ZANZIBAR ATUMA SALAMU ZA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA WA 2013


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Dk Ali Mohamed Shein, akitoa salamu za kuukaribisha Mwaka mpya wa 2013,kwa wananchi wa Zanzibar na Watanzania wote kwa ujumla,pia aliwasihi wananchi kuendela kushirikiana na Serikali yao katika kuendeleza mipango mbali mbali ya maendeleo,na kuwataka kuwa walinzi wa rasilimali pia kuzingatia taratibu za kisheria, kwa kuwa na elimu bora ya rasilimali hizo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA RASMI MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI


Bango linaloonyesha Idadi ya watu wote Watanzania, baada ya kuhesabiwa katika zoezi la kuhesabuSensa lililoanza mwezi Agosti mwaka huu na kufikia tamati hii leo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, alipotangaza rasmi matokeo ya Senza ya watu na makazi na kutaja idadi kamili, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na wananchi wakati akisoma hotuba yake ya kutangaza rasmi uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi, leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Rais Jakaya, alisema kuwa katika Sensa ya mwaka huu, watanzania wameongezeka kwa asilimia kubwa ukilinganisha na Sensa iliyofanyika kwa mara ya kwanza nchini ya mwaka 1967, ambapo Watanzania wote walikuwa ni Milioni 12, 313, 054, na Tanzania Bara walikuwa ni milioni 11, 958,654 na Visiwani Zanzibar, walikuwa ni 354, 400, ambapo baada ya mwaka huo, Sensa kama hiyo ilifanyika tenamwaka 1978, 1988,2002 na hii ya mwaka huu 2012, ambapo imetoa idadi ya Watanzania wote kuwa ni jumla ya Milioni 44, 929,002. 
Baadhi ya Madiwani na viongozi mbalimbali wa Serikali, waliohudhuria katika hafla hiyo leo.
Kikundi cha Uhamasishaji cha Temeke, akikiwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kilichokuwa kikiendelea na kazi yake ya uhamasishaji uwanjani hapo.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kuhudhuria hafla hiyo.
Bendi ya THT, kutoka (kulia) ni Marlow, Amin na Linah, wakitoa burudani jukwaani wakati wa hafla hiyo.
Wananchi wakisebeneka kushangilia baada ya Rais Jakaya Kikwete, kutangaza rasmi matokeo hayo ya Sensa.
Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba, wakati akiondoka katika viwanja vya Mnazi Mmoja, baada ya kuzidua rasmi matokeo ya Sensa ya watu na makazi.

Sunday, December 30, 2012

BREAKING NEEEWZ!! RAIS WA MAKAPERA TANZANIA ISSA KWISSA MWAIFUGE AJIUZULU UKAPERA AWAGEUKA WENZAKE GHAFLA AOA RASMI LEO


 Rais wa Makapera Tanzania, Issa Kwisa Mwaifuge, leo ameamua kuwageuka wafuasi wake rasmi na kuvunja katiba ya kundi lake na kuamua kuuaga ukapera rasmi na kumuoa Binti mrembo aliyewahi kushiriki shindano kubwa la Miss Tanzania, 2004, Verdiana Kamugisha, ambao kwa pamoja wameamua kumeremeta siku ya leo na kufunga ndoa yao katika Kanisa la Lutheran lililopo mitaa ya Sinza jijini Dar es Salaam. Na hapa ni wakati wakiwa katika sherehe ya ndoa yao inayoendelea muda huu katika Ukumbi wa Msasani Makuni. Picha Zote na www.sufianimafoto.blogspot.com
 Bwana Harusi, Issa Kwisa (kushoto) akisebeneka na Suleiman Semunyu, aliyekuwa akipokea zawadi ya keki kwa niaba ya ITV.
 Maharusi, wakipozi kwa picha na wafanyakazi wa Star Tv, baada ya kuwakabidhi zawadi ya keki.
 Hapa ilikuwa ni muda wa Kwaito..........
 Sehemu ya wageni waalikwa.....
 Wadau kutoka (kulia) ni James Range, Joseph Mpangala na Martine Mauya, wakipozi kwa picha mbele ya kamera ya Sufiaimafoto.
 Baadhi ya wafanyakazi wa ITV ambao ni wafanyakazi wenzake na Bwana Harusi, wakipozi kwa picha, baada ya kukabidhiwa zawadi ya keki na Bwana harusi.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Chanel Ten, wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kupokea zawadi ya Keki.
 Sehemu ya wageni waalikwa,..
Salum Mkambala, akisebeneka kwa staili yake wakati akielekea kupokea zawadi ya keki kwa niaba ya wafanyakazi wenzake wa Chanel Ten.