Friday, December 14, 2012

*RAIS KIKWETE AMPOKEA RAIS WA MADAGASCAR ANDRY RAJOELINA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza na mgeni wake, Rais wa Madagascar, Mheshimiwa Andry Rajoelina mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo, kwa ziara ya siku mbili nchini.
Rais Jakaya kikwete (kulia) akiongozana na mgeni wake Rais wa Madagascar, Mheshimiwa Andry Rajoelina baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo, kwa ziara ya siku mbili nchini. Picha na Fredy Maro, Ikulu





KAMPUNI ya Lakeland Africa kesho itaanza safari ya ‘Mtanzania tembelea Tanzania’ kwa siku 14 kwa lengo la kukuza utalii wa ndani na kujenga utamaduni wa Watanzania kutembelea vivutio vya utalii nchini.

Safari hiyo itakayoanzia Mlimani City Dar es Salaam kesho inatoa fursa kwa watanzania kutembelea vivutio mbalimbali ikiwemo Hifadhi ya Saadan, Pangani, Lushoto, Tarangile, Olduvai Gorge, Lake Manyara, Ngorongoro na Serengeti na pia watapata nafasi ya kutembelea kijiji cha Butiama alikozaliwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere na kuzuru katika kaburi lake.

“Lakeland Africa sasa itaendesha safari za namna hii kuhimiza watu kutembelea vivutio vya utalii nchini kwa kauli mbiu ya ‘kuwa mtalii ndani ya nchi yako”

Kuanzia mwezi januari mwakani Lakeland Africa itaendesha safari za kila wiki kwenda hifadhi na makumbusho ya kistoria katika maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwamo Lushoto, Pangani, Saadani, Selous, Kilwa, Bagamoyo na Mikumi

Katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata fursa hii ya kuitembelea nchi yake Lakeland Africa imeandaa ratiba ya mwaka mzima ya safari zote ili watu waweze kuchagua na kupanga safari kulingana mahitaji yao.

Wapigie Lakeland Africa sasa kupanga safari yako ya mwakani, mwezi wowote utaopenda kuzuru na kuwa mtalii ndani ya nchi yako.

metolewa na Lakeland Africa.
+255222-761811
+255784885901
‘Kuwa mtalii ndani ya nchi yako

No comments:

Post a Comment