Thursday, December 6, 2012

WANAHABARI AFRIKA MASHARIKI WANOLEWA JUU YA WAJIBU WA VYOMBO VYA HABARI KATIKA UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA SOKO LA PAMOJA



Mwezeshaji wa mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa Habari juu ya Wajibu wa Vyombo vya Habari katika utekelezaji wa Soko la Pamoja la Jumuia ya Afrika ya Mashariki (EAC), Balozi Jeremy Ndayiziga, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo yaliyoliyoanza leo Jijini Dar es Salaam na kushirikisha waandishi kutoka nchi Wanachama wa EAC. Kulia ni Mtaalam wa Masuala ya Habari kutoka EAC, Sukhdev Chatbar, ambaye pia ni mratibu wa mafunzo hayo. Balozi Ndayiziga ni Mtaalam katika Masuala ya Mtengamano wa EAC.


Washiriki wakichangia mada katika mafunzo hayo ambayo yameandaliwa kwa pamoja kati ya EAC na Shirika la Kijerumani la GIZ.
Washiriki wakifuatilia mada na michango ya washiriki wengine kwa umakini.
Mwandishi Mkongwe, Zephania Ubwani kutoka Mwananchi Communication Ltd,Arusha akichangia mada. Kulia ni Salma Saidi pia wa Mwananchi na DW Zanzibar.
Picha ya pamoja ya washiriki wote na wawezeshaji.
Mtaalam wa Masuala ya Habari kutoka EAC, Sukhdev Chhatbar, ambaye pia ni mratibu wa mafunzo hayo akijadili jambo na Mwanahabari Mkongwe na Mchambuzi wa Masuala ya Siasa za Afrika, Jenerali Ulimwengu. Ulimwengu pia ni Mwezeshaji katika Mafunzo hayo.
Mkufunzi akiendelea na kutoa mada. Kulia ni Mkufunzi Mwenzake Jenerali Ulimwengu akimsikiliza kwa makani na kushoto ni Mshiriki Mwandishi Kimeli arap Kemei kutoka Kenya.


Huu ulikuwa wakati wa Mtengamano kati ya Fiona na James
Mercy na Fiona wakiwa mkutanoni.





Kipande cha barabara ambacho ujenzi wake unaendelea kwa kiwango cha lami kati ya Ndundu mkoani Pwani na Somanga mkoani Lindi chenye urefu wa kilometa 60 sasa umepangwa kukamilika kabla ya mwezi Juni 2013. Taarifa hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Mhe. Eng. Gerson Lwenge wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea mradi huo akitokea mkoani Lindi.


Mheshimiwa Lwenge alimjulisha Rais Kikwete kuwa, baada ya mkandarasi huyo kushindwa kuikamilisha kazi hiyo mwezi Januari 2011 kwa mujibu wa mkataba, taratibu kadhaa zilifuatwa ili kuhakikisha kuwa mkandarasi huyo anachukuliwa hatua stahiki kwa lengo la kuhakikisha anaikamilisha kilometa 28 zilizobaki kama ilivyokusudiwa.
“Hatua kadhaa zimekwishachukuliwa ambapo kwa sasa mkandarasi ameweza kuongeza uwezo kwa kuzalisha kilometa 5 za lami kwa mwezi na hivyo kurudisha matumaini kuwa ndani ya miezi sita kazi hiyo inaweza kuwa imekamilika” alisema Naibu Waziri Injinia Lwenge..
Mheshimiwa Rais aliitaka Wizara ya Ujenzi kupitia Tanroads kuhakikisha kuwa inausimamia mradi huo kwa karibu zaidi ili kuondoa visingizio vingine vyoyote vinayvyoweza kusababisha mradi huo kuchelewa zaidi.
Ujenzi wa sehemu hiyo ya barabara ambayo ndiyo pekee iliyobaki katika barabara kuu inayounganisha mikoa ya Kusini na Jiji la Dar es Salaam, ulianza mwaka 2008 ukiwa umepangwa kukamilika ndani ya miaka mitatu. Mkadarasi aliyeshinda zabuni hiyo ni Kampuni ya M/S M.A. Kharafi & Sons kutoka Kuwait kwa gharama ya Shs. 58.8 bilioni. Fedha hizo zimetolewa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na mifuko ya maendeleo ya KUWAIT na OPEC.Baada ya ziara hiyo Mheshimiwa Rais alirejea Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment