Tuesday, January 15, 2013

HALI ILIVYOKUWA HUKO KIGAMBONI BAADA YA WAKATI WA MAANDAMANO YA WANAFUNZI WA IFM


Wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha (IFM) wakielekea kupanda Difenda huku wakiangukiana baada ya kupigwa mabomu kwenye kituo cha Pilisi Kigamboni walipofika kulazimishwa kufanya, mkutano na Kamanda Kova mbele ya Kituo hicho badala ya Eneo lililoandaliwa kwenye viwanja vya mpira vya Machava.

Wakitumbukizwa kwenye Defenda kwa nguvu baada ya kuzingirwa kwenye jengo la CCM lililopo karibu na Kituo hicho cha Polisi huku wakibubujikwa na machozi kufuatia mabomu ya machozo yaliyopugwa kwenye eneo hilo.

Askari ambae hakuwa kwenye vazi rasmi akimsulubu mmoja wa wanafunzi mbele ya kituo cha polisi baada ya kukataa amri ya kuchuchumaa na kutembea kwa magoti hadi kituoni hapo.

Wanafunzi hao wakielekea kwenye kituo cha polisi huku wakiamriwa kunyoosha mikono juu baada ya kuwekewa mtego na kunaswa pamoja na kupigwa mabomu kutokana na kulazimisha kufanyika kwa mkutano wao na kamanda Kova mbele ya kituo hicho cha Polisi.

Mwanafunzi aliyeshikwa akipandishwa kwenye Difenda.

Kundi hili lilijificha kwenye baa ya CCM iliyopo eneo hilo wakpigwa mabomu na kuchomolewa.

Utakwenda Tu!
Hiki ndicho kikosi Kizima kilicho dhibiti wanafunzi hao ndani ya dakika 15 tu! na wakanyooka
BAADA ya wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha (IFM) kwenda kigamboni ambako Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova kuwataka wakawasilishe hoja zao hukohuko ambako wanadai walipeleka majina ya wahalifu na hayajashughulikiwa, waligoma kufanya mkutano kwenye viwanja vya mpira eneo la Machava nakutaka mkutano huo ufanyike kwenye kituo cha polisi Cha Kigamboni ambako wanafunzi wengi wao walielekea huko.
Mara baada ya kufika kwenye kituo hicho waliamriwa maratatu waondoke waende kwenye mkutano na Kamanda Kova wakakataa baada ya hapo ndipo mabomu yakaanza kupigwa. 
Kwenye mabomu hayo wanafunzi kadhaa walijeruhiwa na kuumia wengine walipoteza fahamu. Hata hivyo walioshikiliwa wote waliachiwa na kutakiwa kwenda kwenye mkutano huo ambao uliazimia mambo kadhaa ya utekelezaji ili kutatua tatizo hilo la wizi kwenye eneo hilo. Kamanda Kova aliwaahidi wanafunzi hao kuwa watapata mrejesho wa hatua walizochukuwa siku ya tarehe 30 mwezi huu.Picha zote na Libeneke la Mtaa kwa Mtaa Blog

No comments:

Post a Comment