Tuesday, January 29, 2013

KINANA NA UJUMBE WAKE WAKAGUA UJENZI DARAJA LA MALAGARASI KIGOMA

Meneja mradi wa ujenzi daraja la Malagarasi wa Kampuni ya Korea ya Hanil, Jung Sik You, (wapili kushoto) akiwatembeza Kinana (watatu kushoto), Migiro (wanne) na Nape (wapili kulia) kwenye mradi wa ujenzi wa dajara la Malagarasi wilayani Uvinza mkoani Kigoma Januari 28, 2013. Daraja hilo linatarajiwa kukamilika miezi mitatu ijayo. Kinana na ujumbe wake wapo mkoani Kigoma kwa ajili ya kushirikji sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM, zitakazofanyika Februari 3, 2013 mkoani.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kushoto) akipata maenezo ya ujenzi wa daraja la Malagarasi kutoka kwa Meneja mradi wa ujenzi daraja hilo wa Kampuni ya Korea ya Hanil, Jung Sik You.
Kinana akizungumza na mwananchi wa Kigoma Amani Mahmoud wakati akikagua ujenzi wa daraja la Malagarasi. kuhsoto ni Meneja mradi wa ujenzi daraja la Malagarasi wa Kampuni ya Korea ya Hanil, Jung You.
Nape akishiriki kupiga ngoma ya kuongoza matembezi kuingia mji mdogo wa Nguruka. Pembeni yake ni Asha Baraka. Matembezi hayo yaliongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk, Asha Rose Migiro na Asha Baraka wakiwa mstari wa mbele kwenye matembezi kuingia mji mdogo wa Nguruka Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma kwenye mkutano wa hadhara wa CCM
CCM SAFI: Wananchi wa Nguruka wakisema wakati msafara wa Kinana wa ujumbe wake ukipita kwa matembezi kuingia katika mji huo mdogo kufanya mkutano wa hadhara
Wananchi husuasan kina mama wakishangilia msafara wa Kinana upoingia Nguruka
Mwanafunzi wa shule ya msingi Nguruka (kulia) akimshangilia Nape akishiriki kupiga ngoma iliyoongoza matembezi kutoka barabara kuu kuingia mjini mdogo wa Nguruka kwa ajili ya mkutano wa CCM, Matembezi hayo yaliongozwa na Kinana
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wa Nguruka baada ya msafara wake kuwasili, Januari 28, 2013, kwa ajili ya mkuytano wa hadhara wa CCM
Dk. Asha Rose Migiro akishangiliwa na mkazi wa Nguruka, Asha Kipenda wakati wa mapokezi ya msafara wa Kinana na ujumbe wake
Dokii akitumbuiza kwenye mkutano wa CCM uliofanyika Nguruka, Januari 28, 2013 ambao ulihutubiwa na Kinana
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akihutubia mkutano wa hadhara wa Nguruka, wilayani Uvinza mkoani Kigoma
Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela akihutubia mkutano huo wa Nguruka mkoani Kigoma
Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Nguruka
Mamia ya wananchi wakimsilikiza Kinana kwenye mkutano huo
Mkazi wa Nguruka akimsikiliza kwa makini Kinana kwenye mkutano huo huku akiwa amepozi kwenye baiskeli yake
Kinana akiwaaga wananchi wa Nguruka baada ya mkutano huo. Pamoja naye ni Dk. Asha-Rose Migiro. Baadaye Kinana na ujumbe wake alienda kwenye mkutano mkubwa mwingine uliofanyika mji wa Uvinza. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO