Tuesday, January 29, 2013

LULU AACHIWA KWA DHAMANA, SASA AENDA "KULA BATA" MITAANI

Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akishuka kutoka katika gari lililomleta leo Mahakama Kuu wakati wa kukamilisha taratibu za kupata dhamana. (Picha na Habari Mseto Blog) 

Lulu akiingia Mahakamani huku akisindikizwa na Askari Magereza
Lulu akiingia mahakamani huku akitabasamu.
Lulu akiingia mahakamani.
Lulu akiwa amezungukwa na baadhi ya waandishi wa habari waliotala kufanya nae mahojiano mfupi baada ya kupata dhamana.
Lulu akiangua kilio baada ya kushindwa kuongea na waandishi wa habari waliokusanyika mahakamani hapo.
Lulu akitoka katika lango Kuu la Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kupata dhamana.
Lulu akilia wakati akitoka Mahakamani huku nyumba akifuatiwa na mama yake mzazi.
Wasanii nao wallijitokeza mahakamani hapo kumfariji Lulu, kulia ni msanii wa filamu, Muhsin Awadh 'Dk. Cheni'
Lulu akiondoka mahakama hapo.
Wakili anayemtetea Lulu akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mteja wake kupata dhamana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo. Lulu amepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali waliosaini bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja, kusalimisha hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam bila ruhusa ya mahakama na kuripoti kwa msajili kila mwezi. Luluanakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.