Saturday, February 9, 2013

MAOFISA HABARI WA SERIKALI WAMALIZA KIKAO CHAO MJINI DODOMA, WATEMBELEA BUNGE NA KUSHIRIKI ZOEZI LA UPANDAJI WA MITI CHUO KIKUU CHA DODOMA.

Mhasibu mkuu msaidizi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Swalehe Chondoma, akishiriki zoezi la upandaji wa miti katika kampasi ya chuo kikuu cha Dodoma.
Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Habari Bw. Raphael Hokororo, akiwafundisha maafisa habari na mawasiliano wa serikali kutoka Wizara, Taasisi, wakala, mashirika ya Umma, mikoa na wilaya upigaji wa picha bora za mnato kwa matumizi ya habari wakati wa kuhitimisha kikao cha maafisa hao mjini Dodoma.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana ambaye alikua miongoni mwa waalikwa waliohudhuria kikao kazi cha maafisa habari na mawasiliano wa serikali akiongea na mafiasa hao mjini Dodoma.
Maofisa habari na mawasiliano wa serikali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Maofisa Habari na Mawasiliano wa serikali wakiwasili Chuo Kikuu cha Dodoma kushiriki zoezi la upandaji wa miti chuoni hapo ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kuhifadhi mazingira ya chuo hicho.
Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akizindua zoezi la upandaji wa miti lililowahusisha mafisa habari wa Serikali katika kampasi ya chuo kikuu Dodoma.
Maofisa habari na Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na zoezi hilo Chuo kikuu cha Dodoma.
Maofisa habari na Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na zoezi hilo Chuo kikuu cha Dodoma.
Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma kufuatia mwaliko wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma kufuatia mwaliko wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

No comments:

Post a Comment