Monday, February 25, 2013

*PROF. YASH PAL GHAI AKUTANA NA WAJUMBE WA TUME YA KATIBA MPYA DAR LEO


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba ya Kenya Prof. Yash Pal Ghai (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Casmir Kyuki (kushoto) na Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume Bw. Joseph Ndunguru katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo. Prof. Ghai amekutana na Wajumbe na kubadilishana nao uzoefu kuhusu uandishi wa Katiba Mpya.
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Prof. Palamagamba Kabudi (kushoto) na Bw. Abubakar Ali (katikati) wakiongea na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba ya Kenya Prof. Yash Pal Ghai katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo, Prof. Ghai amekutana na Wajumbe na kubadilishana nao uzoefu kuhusu uandishi wa Katiba Mpya.

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kulia) na Mjumbe wa Tume Bw. Simai Mohamed (katikati) wakiongea na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba ya Kenya Prof. Yash Pal Ghai katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo. Prof. Ghai amekutana na Wajumbe na kubadilishana nao uzoefu kuhusu uandishi wa Katiba Mpya. Picha na Tume ya Katiba (CRC).