Tuesday, February 5, 2013

WALI WALIWA, MCHELE WACHELEWA, MPUNGA WAPUNGUA.

Niko safarini kuelekea vijiji vya wilayani Sengerma, nikiwa Kamanga napata 'tea' kwa mama ntilie dakika sifuri namwona akijibidiisha kuchambua mchele kwenye sinia, kila punje ya mpunga aliyokuwa akiokota alikuwa akiitupa chini (which means haina kazi tena) kaswali kakaniijia kichwani .... Hivi kama angekuwa na kopo lake la kutupia punje hizo na hasa ukizingatia yeye ni mamalishe na huchambua kuanzia kilo tano na kuendelea kwa siku... baada ya miezi kadhaa si angekuwa na tu'kilo kazaa twa mpunga au pengine ka'debe...? 
Mmmmh Kuuliza si ujinga...