Saturday, February 9, 2013

WAZIRI NCHIMBI AFANYA UFUNGUZI WA SUPER MARKET YA KISASA YA MAGAREZA

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali 
John Minja (kulia) akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk 
Emmanuel Nchimbi (kushoto) kabla ya uzinduzi wa Supermarket ya kwanza 
katika Jeshi la Magereza nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi 
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Supermarket ya kwanza ya Jeshi la 
Magereza nchini.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Military Shop, Afzal Meghji 
akimuonyesha bidhaa mbalimbali zilizopo ndani ya duka hilo, Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi 
akizungumza na maafisa magereza (hawapo pichani) kabla ya kufungua Supermarket 
kubwa ya kisasa ambayo itawawezesha maafisa hao, askari na familia zao 
kupata huduma ya kununua bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu. Kushoto ni 
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, anayefuata ni Mkuu wa 
Jeshi la Magereza nchini, John Minja na kulia ni Mwekezaji Mkuu wa Kampuni 
ya Military Shops ambaye ndiye aliyewekeza katika Supermarket hiyo, 
Sadrunin Virji. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmauel Nchimbi 
akipokea zawadi kutoka kwa mke wa Mwekezaji Mkuu wa Supermakert hiyo, 
Gulshan Virji (kulia).
Mkuu wa Jeshi la Magereza 
nchini, Kamishna Jenerali, John Minja akipokea zawadi kutoka kwa mke 
wa Mwekezaji Mkuu wa Supermakert hiyo, Gulshan Virji (kulia).
Baadhi ya maafisa na askari Magereza wakinunua bidhaa 
mbalimbali katika Supermakert hiyo baada ya kuzinduliwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya 
Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa tatu kutoka kushoto waliokaa), Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (wa 
kwanza aliyekaa kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa mbalimbali 
wa magereza pamoja na wageni waalikwa.