Friday, April 19, 2013

STORI ZA BUNGE APRIL 18 2013


1. Serikali imesema licha ya kupanga Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kutumia teknolojia ya kisasa katika kuhesabu kura kwenye uchaguzi mkuu ujao, kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika nchi za Ghana na Kenya wataweka pia njia mbadala katika kutekeleza zoezi.


Akizungumza Bungeni wakati wa kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu MIZENGO PINDA amesema nia ya NEC kuujaribu mfumo huo ni nzuri lakini ili kuondoa mivutano, Serikali itahakikisha mchakato huo unaendeshwa kwa matakwa ya wadau wote.


PINDA ametolea ufafanuzi huo kufuatia swali aliloulizwa na Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni FREEMAN MBOWE juu ya kutoaminika kwa mfumo wa kiteknolojia unaotarajiwa kutumika na tume ya uchaguzi na namna wadau watakavyoshirikishwa li kujiridhisha nao.
Kivutio kikubwa kilikuwa ni Mbunge wa Kisesa LUHAGA MPINA ambaye ameonesha ukomavu wake kisiasa na kuikosoa Serikali kufuatia kushindwa kutekeleza ahadi zake inazotoa ikiwemo kuwapatia Watanzania wa Vijijini huduma bora za afya.
2. Baada ya ukimya wa miaka miwili, Waziri wa nchi katika ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum Profesa MARK MWANDOSYA ameibuka na kuzungumza bungeni baada ya kupita kipindi cha miaka miwili na kukemea tabia ya baadhi ya Wabunge kuzungumzia masuala ya usalama wa taifa hadharani.
Akitumia fursa hiyo wakati akijibu hoja mbalimbali za Wabunge kuhusiana na michango katika Bajeti ya Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu, Profesa MWANDOSYA amesema usalama wa taifa wako duniani kote hivyo linapojitokeza tatizo ni vema Wabunge wangejifungia ndani kujadili kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge.
Kwenye sentensi nyingine Profesa MWANDOSYA ameshangazwa na kitendo cha Wabunge kutotoa mchango wowote kuhusiana na masuala ya mipango ya maendeleo kwa taifa wakati wakichangia hoja kwenye Bajeti ya Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu.
3. Mbunge mwingine wa Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Kisesa LUHAGA MPINA amekataa kuunga mkono hoja bajeti ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa madai kwamba Serikali imekuwa ikikataa kutekeleza ahadi inazotoa kwa Wananchi wake.
Amesema licha ya utekelezaji wa maendeleo kwa jamii nchini kuhitaji kiasi cha Shilingi Trilioni 16.7 Serikali kupitia Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI imetenga jumla ya Shilingi Bilioni 640, mgao unaoashiria baadhi ya miradi kutofikiwa na fedha hizo.

No comments:

Post a Comment