Friday, May 17, 2013

DIAMOND ATOBOA KWA NINI AMEKUWA KIWEMBE





KWA mara ya kwanza nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond' ameacha gumzo London, Uingereza baada ya kueleza sababu za kwa nini ni kiwembe?


Akifunguka katika mahojiano maalum wiki iliyopita na Kipindi cha Sporah Show cha runingani alipokuwa kwenye ziara ya kimuziki nchini humo, Diamond alizungumza ishu kibao za kimapenzi hasa juu ya msururu wa wanawake ambao tayari ametoka nao.


ASISITIZA ANASUBIRI MTOTO
Kabla ya yote, staa huyo alisisitiza kuwa muda si mrefu anatarajia kupata mtoto kutoka kwa mpenzi wake wa sasa, Peniel Mungilwa ‘Penny’ akimaanisha kuwa ni mjamzito, kinyume na msichana huyo ambaye hivi karibuni alimshangaa Diamond kueneza habari hizo.


KWA NINI ANAPENDA KUBADILISHA WANAWAKE?
Diamond: Mimi ni binadamu kama binadamu wengine wa kawaida. Nampenda mwanamke anayenipenda na kuniheshimu. Ikitokea mikwaruzano huwa mimi nakaa pembeni, natafuta sehemu nyingine. Wakati mwingine mimi ndiye huwa naachwa.


KWA NINI MSURURU NDANI YA KIPINDI CHA MIAKA MITATU?
Diamond: Nikiwa na mtu nikiachana naye naonekana nina matatizo kwa sababu wakati mwingine nakuwa na wanawake wenye majina. Siwezi kukaa bila uhusiano na nakuwa wazi kwa sababu lazima itajulikana tu na kuandikwa kwenye magazeti. Kuna kipindi nilikaa miezi sita bila kufanya kitu chochote (mh!). Lakini nikianza (uhusiano), nikihama naonekana msumbufu.


KWA NINI MASTAA, TENA MARAFIKI?
Diamond: Huwa sitoki, nakuwa nyumbani tu, nakaa na mama yangu (Sanura Kassim ‘Sandra’) nampikia. Nikitoka nakwenda kwenye shoo au studio. Huko ndiko nakutana nao (mastaa wa kike).


ALIMPATAJE JOKATE (MWEGELO)?
Diamond: Alikuwa anazindua nguo zake (Kidoti) akaniomba nikapite nazo kwenye onesho la mavazi, nikapita nazo jukwaani. Baada ya hapo na mimi nilimuomba nifanye naye video ya wimbo wangu (Mawazo), ndiyo ikatokea kama hivyo.


NINI KILIMVUTIA KWA PENNY?
Diamond: Kwanza mimi nilimjua Penny kabla ya Wema (Sepetu), alikuwa mshikaji wangu. Ni mwanamke mzuri, wa kileo, ana akili adabu na heshima. Anampenda mama yangu na familia yangu ‘coz’ na mimi nampenda mama yangu (sifa ambazo kwa mujibu wake Wema alizikosa).


KWA NINI ALIMREKODI WEMA?
Diamond: Kila binadamu anajiona yupo sawa na anaonewa. Sipendi kuongea, nitazungumza vibaya. Mapenzi yanaumiza na mimi naumia pia lakini watu wanadhani mimi ndiye muumizaji. Unamwambia mtu kwa nini una mwanaume mwingine.

Anakuzuga sijui ni pedeshee anampa pesa. Mara unamwona na mwanaume mwingine. Mimi siyo maskini lakini sasa mara unamwona na brazameni mwingine ‘then’ washkaji wanakwambia. Wewe unajifanya kuziba masikio mara unasikia ana mwanaume mwingine. Lakini ikafika wakati nikajikuta naumia sana kwenye mapenzi.

Kama ukisikiliza ule wimbo wa Kesho ni kweli kabisa. Mimi nikakaa pembeni hadi nilipompata huyu wa sasa (Penny).
Nakumbuka (Wema) alinipigia simu akadai mimi ndiye nasema anataka turudiane. Nilikuwa kwenye gari, nikamuuliza anataka nini?

Wakati huo nilishafika nyumbani kwa baby wangu. Nikamwonesha ona sasa, anasema mimi ndiyo nataka nirudiane naye, anatangazia watu hadi saluni kuwa nataka kurudiana naye na kujidai kwenye vyombo vya habari kuwa ananipenda. Kumbe ana wengine (ving’asti) kama ishirini anawahonga (mistari ya wimbo wake wa Nataka Kulewa).


Nilimpa baby wangu akamwambia kistaarabu tuache tulale. Sasa kuna mtu wetu wa karibu ndiye aliyehusika kusambaza ile sauti.


SEMA UKWELI, ULILALA NA UWOYA?

Diamond: (kicheko) Ningeanzia wapi? Unajua mimi ni simba kwa hiyo nikionekana na swala inajulikana lazima nimle hata kama tumeenda sehemu tu kuzungumza ishu za kazi.

KWA NINI WANAWAKE AU ENZI ZILE HAKUWA NA ‘CHANSI’ SASA AMEPATA?
Diamond: Ukimuelimisha mwanamke mmoja umeelimisha ulimwengu mzima. Nawapenda sana, wanajaa tele kwenye shoo zangu. Kilichotokea kwa Wema ilibidi tu sikuwa na jinsi.

ANATAKA MWANAMKE WA AINA GANI?
Diamond: Ukimuuliza mwanamke aliyewahi kuwa na mimi atakwambia najua mapenzi, najua kupetipeti, najua kubembeleza, najua kujifanya mjinga. Narudia tena, awe mzuri, wa kileo, mwenye akili, anayejiheshimu, ampende mama yangu kama mimi ninavyompenda mama yangu.

KWA NINI KIWEMBE?
Uchunguzi uliofanywa ulibaini kuwa chanzo cha staa huyo aliyetokea Tandale, Dar kuitwa kiwembe ni kutokana na tabia yake ya kubadilisha wanawake kama nguo.


Baadhi ya aliowahi kuripotiwa akidaiwa kutoka nao ni Rehema Fabian (Miss Kiswahili 2009), Jacqueline Wolper (msanii wa filamu), Upendo Moshi ‘Pendo’ (Mshiriki wa Maisha Plus) na Natasha (Video Queen wa Bongo Fleva).

Wengine ni Wema (mwigizaji), Jokate (mwigizaji), Aunt Ezekiel (mwigizaji), Najma (msanii wa Bongo Fleva), Penny (mtangazaji DTV), Irene Uwoya (mwigizaji) na wengineo.

No comments:

Post a Comment