Mkurugenzi wa Michezo wa Hoteli za Misali na Ocean View Said Kumbi, akimkabidhi seti za Jezi Nahodha wa Timu ya Waandishi wa Habari za Michezo Zanzibar (TASWA Zanzibar FC) Ishaka Omar, makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani, ikiwa ni udhamini wa timu hiyo.
Meneja Mkuu wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Jacob Mahumbi(kulia) akimkabidhi seti ya Jezi Nahodha wa timu ya TASWA Zanzibar FCIshaka Omar Seti za jezi za mazoezi kwa ajili ya timu hiyo.
Meneja Mkuu wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Jacob Mahumbi(kulia) akimkabidhi seti ya Jezi ,mipira na net za magoli Nahodha wa timu ya TASWA Zanzibar FCIshaka Omar.
Mkurugenzi wa Michezo wa Mahoteli ya Misali Pemba na Zanzibar Ocean View Zanzibar Said Kwimbi, akizungumza katika sherehe hizomza kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Waandishi wa Habari za Michezo Zanzibar (TASWA FC) ili kuendeleza michezo katika visiwa vya Zanzibar na kuitangaza katika midali ya michezo Ulimwenguni.
Mjumbne wa Bodi ya Wadhamini wa timu hiyo ya TASWA FC, akitowa nasaha zake kwa waandishi kuirejesha Zanzibar katika medali yake ilipokuwa ikitajika wakati wa mashindano ya Goseji Zanzibar ilikuwa ikiwika katika Soka Afrika Mashariki.
Meneja Mkuu wa Mahoteli ya Misali na Zanzibar View Jacob Muhumbi, akiipongeza timu hiyo kwa hatua iliofikia na kuhamasisha mchezo wa mpira wa miguu Zabnzibar kwa kutumia kalamu zao kuitangaza Zanzibar kimichezo ndani na nje ya Zanzibar.
Mwenyekiti wa Timu ya TASWA Zanzibar FC Mwinyimvua Abdi , akitowa shukrani kwa udhamini uliotolewa na Mahoteli hayo yanayomilikiwa na Mfanyabiasha Amani Makungu, udhamini huu watautumia vizuri na kufanikisha kiwangi cha mpira Zanzibar kinarejea hadhi yake na Zanzibar kutaja katika Michezo ya Kimataifa na Kitaifa.
No comments:
Post a Comment