Tuesday, May 28, 2013

KILICHOMUUA NGWEAR HIKI HAPA


Taarifa ambazo Lenzi ya Michezo imezipata kutoka Afrika ya Kusini kwa HusseinOriginal ambaye yupo Pretoria, amesema Ngwear amefariki leo asubuhi kwenye gheto ambalo alikuwepo pia msanii M to The P ambaye yeye amelazwa hospitali akiwa mahtuti. 


"Tulivyokwenda kuwagongea asubuhi tuliwakuta Ngwear amefariki na M To The P akiwa amepoteza Fahamu Kabisa"


Baada ya kuwapeleka hospitali Daktari alitibitisha amekufa na ameshatoa taarifa kwa watu wa Karibu wa Ngwear huko Afrika nya Kusini.


Ngwea akiwa na msanii M to the P walitakiwa kurudi Dar leo lakini waliwakuta wamezimia kwenye chumba wote wawili baada ya kuzidisha (overdose) madawa ya kulevya na M to the P.


Hata hivyo mama yake Ngwear ambaye yupo nyumbani kwao Morogoro amethibitisha kupokea taarifa ya kifo cha mwanae na kusema kuwa taarifa za kuwa za kuwa alikuwa Afika ya Kusini alikuwa hana kwani mara ya mwisho kuongea naye zimepita wiki mbili sasa.


Pia amesema taratibu za maandalizi ya mazishi yatakavyokuwa yataanza baada ya kufika baba yake mdogo Ngwear ambaye yupo mkoani Ruvuma kwani anatarajiwa kuwasili kesho Morogoro.

1 comment:

  1. I am really enjoying the thеme/design οf уоuг web
    site. Do you evеr run into anу browser compatibility prοblems?

    A handful of my blog visitorѕ have complaіned about my ѕite not opеrating corrесtly in Explorer but looks great in Safari.
    Do you have any recοmmendations to hеlp fiх
    thіs pгoblеm?

    Visit my web-site: natural breast enlargement

    ReplyDelete