Tuesday, July 2, 2013

MICHELLE OBAMA AMFAGILIA MAMA SALMA KIKWETE KWA KUWAPA ELIMU BURE WATOTO WA KIKE

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mke wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama pamoja na Mama Laura Bush, mke wa Rais Mstaafu wa Marekani Mheshimiwa George Bush kwenye hoteli ya Serena tarehe 2.7.2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe George W. Bush na Mkewe Laura na Mama Salma Kikwete wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wake wa marais wa Afrika Mashariki leo July 3, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Na Anna Nkinda - Maelezo 
Mke wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama amempongeza Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwa kazi kubwa anayoifanya ya kutoa elimu bure kwa watoto Wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi .
Mama Obama alizitoa pongezi hizo leo wakati wa majadiliano baina yake na Mama Laura Bush kwenye mkutano wa wake Wa Marais Wa afrika unafanyia katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mama Obama alisema kuwa wake Wa Marais wanakazi kubwa ya kuhakikisha kuwa wanawasaidia wanawake na watoto hasa katika upatikanaji Wa elimu na mahitaji mengine muhimu.
"Jana nilitembelea makumbusho ya taifa, nilikutana na watoto ambao baadhi yao walikuwa ni wale wanaosomeshwa na Mama Kikwete , niliongea nao watoto hawa wanapatiwa bure elimu, chakula na maladhi hakika nampongeza sana kwa kazi nzuri anayoifanya", alisema Mama Obama.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mama Kikwete alisema kuwa wake wa Marais waliohudhuria mkutano huo wanawawakilisha wanawake wa Afrika 
ambao wanahitaji kusaidiwa katika mambo ya afya, elimu na ujasiriamali.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa katika mkutano huo washiriki watapata nafasi ya kubadilishana ujuzi wa kazi na kutembelea hospitali ya Kansa ya Ocen Road,kituo cha Mabinti na hospitali ya CCBRT ambako watajionea jitihada kubwa zinazofanywa na watanzania za kuisaidia jamii inayowazunguka.
Alisema kuwa baada ya kumalizika kwa mkutano huo anaamini kuwa washiriki watarudi katika nchi zao na kuweza kukubaliana na Serikali zao pamoja na wadau Wa wengine kuwekeza zaidi kwa wanawake ili kuimarisha bara la Afrika.
Mkutano huo wa siku mbili umeandaliwa na Taasisi ya Rais mstaafu wa Marekani George Bush na kuhudhuriwa na baadhi ya wake Wa Marais wa Afrika na Mke wa Waziri mkuu mstaafu Wa Uingereza Cherie Blair.
Mada kuu ni wekeza kwa wanawake imarisha Afrika lengo l ikiwa ni kuimarisha upatikanaji wa Afya kwa wanawake, upatikanaji Wa elimu na uchumi katika Afrika.

No comments:

Post a Comment