Tuesday, September 17, 2013

BAADA YA KUTWAA UBINGWA WA DUNIA FRANCIS CHEKA AMUA KURUDI SHULE ..KIDATO CHA KWANZA


Bingwa wa dunia wa WBF Francis Cheka ambaye hivi karibuni alipewa zawadi ya kiwanja na Rais Jakaya Kikwete baada ya ushindi wake dhidi ya bondia wa Marekani, ameamua kurudi shule.Cheka anasema hakupata nafasi ya kwenda shule kutokana na matatizo ya kifamilia na kuishia darasa la saba. “Mimi sikusoma niliishia darasa la saba, lakini nimeamua kurejea darasani baada ya kupewa udhamini na shule ya St Joseph”.
“Nahitaji kuwa Cheka mpya kielimu ili nifike mbali, miaka kumi ijayo hadi namaliza elimu yangu nitakuwa na miaka 41. Hapo nitaamua niendelee na ngumi au nifanye biashara zangu nyingine “.Habari kamili ipo kwenye gazeti la Mwananchi la Sept 17