Tuesday, September 3, 2013

DADA AKUMBANA NA OPERATION YA KUWAVUA WAVAA VICHUPI MTAANI-AOKOLEWA NA TRAFIC

Khatimu Naheka aliyekuwa Arusha
VIJANA wamechoka kuwaona wanawake wanaovaa kihasarahasara ‘vichupi’ mitaani ambapo wameanzisha oparesheni maalum ya kuwavua kabisa ili watembee utupu ijulikane moja.
Habari hii inathibitishwa na tukio la mrembo ‘miss’ (jina lake halikupatikana) ambaye amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukumbana na kasheshe zito kutoka kwa wanaume kufuatia kinguo kifupi alichokuwa amevaa, kilichoacha nje sehemu kubwa ya mapaja.
Vijana wa mjini wakimvua kitenge alichojistiria mrembo huyo.
JIJINI ARUSHA
Tukio hilo lililovuta umati mkubwa ambalo lilishuhudiwa na shushushu wetu, lilijiri maeneo ya stendi ya mabasi madogo jijini Arusha, wiki iliyopita wakati mrembo huyo akiwa na marafiki zake watatu wakirandaranda kufanya ‘window shopping’.
Mara baada ya kufika eneo hilo, miss huyo alijikuta akizungukwa na wapiga debe wa daladala na kuanza kumshushia maneno makali wakimwambia kuwa wamechoshwa kuona nyeti zao.
Trafiki wakiwa na mrembo huyo baada ya kumwokoa kutoka mikononi mwa vijana.
AVULIWA
Huku sistaduu huyo akidhani ni kelele za kawaida, wapiga debe hao walimzingira na kuanza kumvua kigauni hicho cheusi.

APEWA KITENGE
Mrembo huyo alipoona mambo yameharibika huku wenzake wakitoka nduki, alilazimika kukimbilia katika duka moja la nguo maeneo hayo na kuomba msaada ambapo alisitiriwa kwa kupewa upande wa kitenge kwa msaada wa trafiki wa kike aliyemuokoa.
Kabla ya kusaidiwa na trafiki mwingine wa kiume, yule wa kike alimshauri kuvaa kitenge hicho na kuondoka eneo hilo.
...Trafiki akimhoji.
AKIMBIZWA
Cha kushangaza, wakati anatoka katika duka hilo hali ilizidi kuwa tete baada ya midume walioonekana kuchoshwa na uvaaji wa nguo fupi kumkimbiza na kuanza kumvua kitenge hicho hivyo kusababisha vurugu kubwa kiasi cha matrafiki kadhaa kuingilia kati na kuwatawanya vijana hao.
Trafiki akimpeleka mrembo huyo kwenye gari.
AJITETEA
Wakati dada huyo akihojiwa na matrafiki hao, alijitetea kuwa anawashangaa vijana hao kwa kumfanyia vurugu wakati nguo hiyo siyo fupi na mara nyingi amekuwa akiivaa na kutembea nayo maeneo kama hayo bila kupata tatizo lolote.
“Afande hii nguo huwa naivaa sana na sijawahi kupata matatizo yoyote, sijui leo imekuwaje lakini siyo fupi kama wanavyodai, nimevaa na kitenge lakini bado wananifanyia vurugu,” alilalamika dada huyo kwa uchungu.
Licha ya dada huyo kuwa katika mikono ya mmoja wa matrafiki wa kiume, jamaa hao walizidi kumfuatilia huku wakimrushia maneno makali ya matusi na wakati mwingine kumsukuma.
Baada ya trafiki huyo kuona hali inazidi kuwa mbaya, alisimamisha gari moja la serikali na kumuombea lifti kwa lengo la kumnusuru kufanyiwa kitu mbaya.
..Mrembo akipanda kwenye gari.
TUMEWACHOKA
Wakizungumza na gazeti hili juu ya tukio hilo, ‘machalii’ hao walisema kuwa wamechoshwa na uvaaji mbovu wa baadhi ya akina dada ambapo sasa wameamua kuwafanyia vurugu hizo mpaka hapo watakapoacha kuvaa hovyo.
“Tunakushukuru kwa kupiga picha, wanatuchosha hawa dada zetu, nguo wanazotuvalia barabarani ni za kuvaa nyumbani tena chumbani lakini wao wanavaa sehemu kama hizi, kuanzia sasa kazi itakuwa kama hii hadi watakapoacha, dawa yao ni kuwawashia moto,” alisema mmoja wa wapiga debe hao huku akisapotiwa na wenzake.
Siku za nyuma mchezo wa kuwavua nguo fupi wanawake ulisaidia kupunguza tabia ambapo kwa sasa imerejea kwa kasi hivyo ili wanusurike na adha hiyo ya kuvuliwa hadharani inayoshika kasi, inabidi kuvaa kiheshima