Monday, September 30, 2013

JEMBA YACHEZEA KICHAPO NA CHANGUDOA BAADA YA KUPEWA BILA KULIPA

Denis Mtima na Irene Profil
WAKATI Oparesheni Fichua Maovu (OFM) inayoendeshwa na Global Publishers ikiwa mzigoni, imenasa tukio la fedheha kwa njemba mmoja akichezea kichapo ‘hevi’ kutoka kwa wanawake waliosadikiwa kuwa machangudoa.
Katika tukio hilo lililojiri hivi karibuni majira ya asubuhi, maeneo ya Afrika Sana jijini Dar, jamaa huyo alidaiwa kuopoa changu ambaye alikwenda kumpa ‘mambo’ ya kiutu uzima kisha wakazinguana.
Mashuhuda wa tukio hilo ambao kwa sehemu kubwa walikuwa ni madada poa, walidai kuwa baada ya jamaa huyo kupewa huduma ya penzi jirani na eneo hilo aligoma kulipa hivyo timbwili zito likaibuka.

Ilidaiwa kuwa wakati jamaa huyo akitoka nduki, wanawake hao waliounda umoja wao walipiga kelele za mwizi na kusababisha wenzao waliokuwa jirani kufanikiwa kumdhibiti kisha kumpa kichapo huku wakimchania nguo na kuzua taharuki kubwa.
Pamoja na kufurukuta, jamaa huyo alishindwa kuhimili mangumi ya wanawake hao waliokuwa na hasira ya ajabu hadi akajikuta akitokwa na kijasho chembamba kabla ya kufanikiwa kuwakimbia.
Akizungumza na OFM, dada huyo aliyegoma kujitambulisha alisema kwamba jamaa huyo aligoma kutoa kiasi cha fedha walichokubaliana (aligoma kutaja) kabla ya kwenda kufanya mapenzi.
“Haiwezekani mtu tumekubaliana vizuri na amepata huduma safi, iweje agome kutoa mtonyo (fedha)? Hii ni kazi kama kazi nyingine kwa nini asiiheshimu? Anadhani mimi nitakula wapi wakati ajira zenyewe wanapeana wakubwa?” alihoji mwanamke huyo huku akiondoka eneo hilo baada ya kutulizwa mizuka na wenzake.