Tuesday, September 3, 2013

Mabadiliko ya tabianchi yaeneza magonjwa

Uchunguzi mpya uiliofanywa na wataalam kutoka vyuo vikuu vya Exeter na Oxford Uingereza umebaini kuwa mabadiliko ya hali ya anga yamekuwa chanzo kikubwa cha kuenea kwa wadudu waharibifu pamoja na magonjwa ya mimea.

Wadudu hao wanaenea kwa umbali wa takriban kilomita 3 kila mwaka.
Wachunguzi hao wanasema wadudu hao wamekuwa wakisafiri kuelekea maeneo ya Kaskazini na Kusini , mahala ambapo awali pamekuwa na baridi kali.

Utafiti huo umechapishwa katika jarida la kisayansi lijuilikanalo kama Nature Climate Change.

Inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 10 na asilimia 16 ya mavuno kote duniani yanaharibiwa na milipuko ya magonjwa. Wataalamu wanaonya kuwa kuongezeka kwa viwango vya joto duniani huenda ukafanya hali hii kuwa mbaya zaidi.

Daktari Dan Bebber, mmoja wa wachunguzi kutoka chuo kikuu cha Exeter alisema: '' upatikanaji wa chakula duninai ni mojawapo ya changamoto kuu itakayotukabili katika miongo michache ijayo''

Aliongezea kuwa:'' hatutaki kupoteza mazao kwa wadudu na magonjwa''

Kwa sasa inadhaniwa kuwa asilimia 10 na 16 ya mimea kote duniani huharibiwa na magonjwa. Watafiti hao wanaonya kuwa kuongezeka kwa viwango vya joto duniani huenda ikafanya hali kuwa mbaya zaidi.
Uchukuzi katika Biashara.

Katiuka kuchunguza tatizo hilo kwa undani, wataalamu hao walidadisi aina ya wadudu 612 na magonjwa ambayo yalikusanywa kutoka sehemu mbali mbali duniani kwa muda wa miaka hamsini iliyopita.

Baada ya utafiti huo, Daktari Dan Bebber wa Chuo Kikuu cha Exeter alisema, '' tumebaini waziwazi kuwa ongezekao la joto linachangia mabadiliko haya''

Kumekuwa na ongezekao la kuvu na ugonjwa unaoathiri ngano ambao umehatarisha mazao barani Afrika, Mashariki ya Kati na bara Asia , wadudu kama kombwamwiko maarufu kama Mountain pine Beetle wamekuwa wakiharibu miti nchini Marekani, kwa kueneza bakteria, virusi na minyoo.

Wadudu hao wanaenea kwa mwendo tofauti tofauti, vipepeo na wadudu wengine wanasafiri hata umbali wa kilomita 20 kwa mwaka, lakini bakteria husalia pale pale.

Wadudu hao wanaenea kutoka ikweta hadi kwenye ncha ya Kaskazini na Kusini. Biashara ya kuuza mazao kati ya nchi mbali mbali pia huchangia kueneza wadudu hao.

Daktari Dan alisema inabidi sehemu za mipaka zifanyiwe ukaguzi kuzuia kuenea kwa wadudu kati ya nchi jirani , na mazao yaliyoathiriwa kuwekwa sehemu za kipekee.

No comments:

Post a Comment