Tuesday, October 22, 2013

KANIPA DEADLINE EITHER NIKAJITAMBULISHE KWAO AMA TUACHANE KIMOJA..HELP

Nimekuwa kwenye uhusiano na mpenzi wa roho yangu kwa takriban miaka mitatu.
Kwa kipindi chote hicho tumekuwa tukiishi mikoa tofauti. Yeye anafanya kazi Babati na mimi nafanya kazi Dodoma.
Licha ya umbali uliopo tumeishi kwa upendo na kuaminiana na hata ndugu na wazazi wanajua kuhusu uhusiano wetu tukitarajia kuja kufunga ndoa baadae. 
Siku za karibuni amekuwa akisisitiza sana nikatoe mahali kwao nami nikawa namuambia sawa tutafanya hivyo na nimemueleza sababu ya kuchelewa ni matatizo ya kifamilia yanayonikabili.
Ghafla wiki iliyopita alikata mawasiliano na hataki pokea simu yangu wala kujibu sms.
jana nimekaa nawaza akanitumia sms kuwa nadhani nishaamua kama namhitaji niende kwao Marangu kabla ya tar 25 mwezi huu vinginevyo simuhitaji.

Kweli nimeishiwa nguvu kwa kuwa sidhani kama kwenda kwao kwa kuforce kwa deadline ni vyema. Anajua kuwa nampenda sana lakini sasa hakuna my love wala sweet.. Ni mwendo wa hey na hello yan full ubabe. Nishaurini wakuu maana natarajia kwenda lakini kwa sasa sijajipanga kusema kweli.