Tuesday, October 8, 2013

SIMUELEWI BINTI HUYU, AMENITENDA ILA BADO ANANING'ANG'ANIA

Kuna binti (mwanachuo) ambaye tulikubaliana kuwa baada ya miaka kadhaa tutaunda kafamilia ketu, Baada ya miaka miwili ya mahusiano yetu (march 2013) nilipata tatizo la kusimamishiwa mshahara na ndani ya kipindi hicho huyo mrembo(aliyekuwa mchumba wangu) aliniambia kuwa anashida ya pesa, Nami kwa kusema ukweli sikuwa na kitu na ningefanyaje hali ya kuwa nishazoea kukinga kwenye ATM mashine tu! Nikampa ukweli kuwa nimevamba kwasababu sina mshahara ila hakuniamini, Akaanza kuniropokea maneno mi nikamwambia "usinisumbue kwani we si una wazazi na wanajua uko chuo? Waambie wakutatulie tatizo lako kama kweli ni la msingi."
Na ukweli wazazi wake hawana njaa sana. Ila baada ya hapo mawasiliano hayakuwa mazuri nami sikumfatilia kwasababu nilimuona sio muungwana, Yeye alikuwa ananipigia mara chache lakini maongezi yalikosa utamu ule uliozoeleka. Mwezi wa nane nilihudhuria mafunzo fulani yaliyonilazimu ninunue modem ya Airtel hivyo nikapata namba mpya ya simu na kwakuwa nilijiunga na vifurushi ktk laini hiyo mpya nilikuwa na muda na sms za kutosha. Jion moja nikamtext "Niambie mke wangu?" Akanijibu kwa ukali lkn nikamzingua had akawa mlain japo hakunijua mimi nani. Tukaendelea kuchat had ukafika muda nikamlazimisha aniambie mimi ni nani maana alishaniambia yeye ana mume mmoja ila alipotaja jina nusura chozi linitoke kwani alinitajia jina tofauti na langu. Nikakaa kidogo nikampigia aliposikia sauti yangu akapatwa na bumbuwazi akakata simu, nikampigia tena akapokea lakini hakuweza kuongea la maana alianza kulia huku akiniambia huyo aliyenitajia ni jamaa mmoja wa first year(ye ni 2nd yr). Alimtongoza tu walikuwa wanawasiliana na anamuita mumewe,baby ili tu amnyenge pesa zake ila hajasex nae hivyo nisiamue lolote. Niliamua kumpuuzia toka siku hiyo ila bado ananisumbua anaomba nimsamehe ili tutimize lengo letu. Kinachonisumbua zaidi sikubahatika kufanya maamuzi ya wazi nimekaa kimya tu nausikilizia upepo japo maisha bila mpenzi nimeyaona ya amani ila hayana furaha.


SASA WAUNGWANA NIPENI MAWAZO YENU: