Tuesday, November 12, 2013

BAADA YA KUONA PICHA YAKE YA UTUPU KILIO CHA KWIKWIII

HUU NDO MKASA AMBAO HUSNA HATAUSAHAU MAISHANI MWAKE.........HILI NDO SIMULIZI LALE BAADA YA PICHA ZAKE ZA UTUPU KUSAMBAA....
------------------------------------------------------------------
“Ni kweli ni picha zangu, nilipigwa na boyfriend wangu wa zamani, Frank ambaye ni mdogo wake Queen Suzy (Suzan Chubwa). Najuta sana kukubali kupiga,” alisema huku akimwaga 
machozi.
“Kipindi nikiwa na Frank, niligundua ana mwanamke mwingine nikamwambia aachane naye, lakini nikaambulia kipigo. Hata mama yangu alikuwa hataki mimi niwe naye maana alikuwa akinigeuza ngoma kwa kipigo.
“Niliongea na wifi Suzy (Queen) akasema atazungumza naye, lakini haikusaidia kitu. Nikaamua kuachana naye. Ndipo aliponipigia simu na kuniambia atanifanyizia kwa sababu alikuwa na picha zangu za utupu.

“Kwa kuhofia aibu, nikakubali kurudiana naye, lakini tabia zake zikazidi kunichefua, baadaye nikaachana naye jumla. Alinipigia simu kunitisha kuwa akinikuta na mwanaume mwingine atanishikisha adabu, lakini sikujali.
“Kuna wakati alinipigia simu na kunieleza kuwa flashi iliyokuwa na picha zangu za utupu pamoja na Mary (aliyekuwa mpenzi wa Frank ambaye naye alipigwa picha kama hizo) imepotea.

“Nilipombana kuhusu mazingira ya kupotea hakuwa na maelezo yanayoeleweka, sikutilia maanani, nilipopigiwa simu na kuambiwa kuwa kuna picha zangu za utupu nilikumbuka maneno yake... mimi nahisi ni Frank atakuwa amecheza mchezo huu,”alisema Husna akiendelea kumwanga machozi.