Friday, December 27, 2013

MKE WANGU ANANIPANGIA RATIBA ZA KUFANYA NAE MAPENZI...!! USHAURI JAMANI NIFANYEJE...??

Habari yako Mnyetishaji...
Mimi ni Kijana wa miaka 29 , Nimeoa miaka mitatu iliopita , kabla sijaoa nilikuwa najua nikishaoa na kuwa na mke wangu ndani issue ya matamanio ya kimwili itakuwa hainisumbui kwa kuwa nitakuwa na mke ndani kila nikitaka kitu napata, lakini imekuwa kinyume na nilivyofikiria..kwani nimekuwa mtumwa mke wangu ananipangia siku gani tufanye mapenzi kwa week mara 2 tu , siku zingine hataki kufanya chochote na mimi na nikilazimisha tunagombana na kutishia kuniacha...

jamani hii ni sawa ?
je nifanyaje? ama nitafute demu wa nje?