Friday, December 27, 2013

TETESI:MWANADADA JACK CLIFF AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA MACAO/CHINA


Jackie Cliff ambaye ni video queen wa Bongo anadaiwa kukamatwa na dawa za kulevya nchini China. Star mmoja nchini aliyekataa kutajwa jina lake aliutonya mtandao wa swahiliworldplanet bila kufafanua zaidi kwa kusema kuwa Jackie amekamatwa na madawa ya kulevya China:

"Jackie Cliff amekamatwa na unga China". alisema star huyo huku akitutumia na picha za mwanamke aliyefungwa kitambaa usoni baada ya kukamatwa na dawa hizo na mwanamke huyo anadaiwa ni Jackie Cliff. Angalia picha hizo hapo chini..........

Hata hivyo baadhi ya mitandao jana iliweka habari za mwanamke mmoja wa kitanzania kukamatwa na dawa za kulevya huko china lakini bado habari hizo hazikubainisha mwanamke huyo ni nani na usiku huu ndiyo ikasemekana ni Jackie Cliff. Habari hiyo inasomek kama ifuatavyo: 

"Mwanamke wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 amekamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao. Dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na jumla ya vidonge 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720.

"Mwanamke huyo alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne iliyopita. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko Chima.

"Pichani ni mwanamke huyo wa Kitanzania (akiwa amefunikwa uso) aliyekamatwa na kilo 1.1 za heroin huko Macau. Hapo amepigwa picha na vidonge vyake kwenye press conference huko Macau, Disemba 19, 2013."