Monday, January 6, 2014

MAENDELEO YA MSIBA WA MPENDWA WETU ZAINAB BUZOHERA


Zainab Buzohera enzi ya uhai wake.

Harambee ya mpendwa wetu Zainab Buzohera ilifanyika Jumapili January 5, 2014 wanaDMV wamechangisha $ 22, 938 kuwezesha kusafirisha mwili wa marehemu Tanzania kwa mazishi gharama za kusafirisha mwili zilikuwa $15,000 kwa watu waliombali na DMV ambao bado wangependa kutoa rambirambi zao mnaweza kutoa kupitia Ms Ngalu Buzohera CITI BANK AC 50070000 Routing 9106834936 au Yusuf Buzohera Bank of America AC 005779974019

Kisomo Kitafanyika kesho Jumanne Jan 7, 2014 kuanzia saa 11 jioni (5pm) sehemu itakapofanyika tutawajulisha baadae

Mwili wa marehemu unatarajiwa kuondoka siku ya Jumatano Jan 8, 2014 kwa mazishi Tanzania

Kwa maelezo zaidi na maelekezo

Ngalu Buzohera 240 330 0169
Idd Sandaly 301 613 5165
Jabir Jongo 240 604 0574
Jasmine Bernett 410 371 9966
Hidaya Mahita 240 271 7799
Catherine Mukami 240 481 0392
Irene Milembe 571 501 0122
Latifa  Mzese 240 603 7363

Kwa niaba ya familia Uongozi wa DMV unapenda kuwashukuru watu wote waliojitokeza kwenye harambee wakiwemo Watanzania wenzetu wa New York na wengine wote popote pale mlipo kwa nia moja au nyingine mmeonyesha Upendo, mshikamano, ushirikiano na kikubwa Utanzania mbele daima, pamoja na kuondokewa na mpedwa wetu kamwe hamkutetereka, mlisimama imara. Tunawashukuru sana kwa moyo wa upendo mliouonesha. Dullah na familia ya Buzohera inasema asante bila kusahau vyombo vya habari vimefanyakazi kubwa usiku na mchana tangia siku mauti ilipomkuta mpendwa wetu tunawashukuru sana hatuna neno au kitu cha thamani tatakacho walipa kitakacholingana na hili kubwa mlilolifanya kwa mpendwa wetu zaid Tunasema asantei na mwenyezi Mungu mwingi warehema awazidishie saba mara sabini.