Friday, January 10, 2014

SANAA SIO KUKURUPUKA ALISEMA ''YUSTER NYAKACHARA'


'Yuster Nyakachara' 'Bongo Movie's Actress'

Msanii huyu amefunguka kuhusu kilichomvutia kuanzisha Kampuni ya filamu iitwayo EAGLE ENTER TIMENT kuwa sio kufuata mkumbo wa waliofungua kampuni bali yalikuwa malengo kama malengo mengine katika biashara zingine, Hakuishia hapo aliendelea kusema kwamba sanaa sio kitu cha kukurupuka inahitaji kipaji na ubunifu wa hali ya juu, 


Hivyo yeye hajutii kudumbukia kwenye Tasnia ya filamu maana hio ni
kazi aliojipangia mwenyewe kwamba ipo siku atadumbukia kwa miguu miwili na ndio tayari amshadumbukia.


Ni matumaini yake kuwa atawabeba wasanii chipukuzi kwa moyo mmoja mradi tu wawe na vipaji vya ukweli, Yuster alisema kwa sasa hatosema mengi anasubiri wadau muone kwanza kazi yake aliyocheza na kuwashirikisha waigizaji nyota hapanchini,


Hapo ndipo mtakapojua kuwa anachokisema ni kweli au laa?