Thursday, March 13, 2014

MWILI WA MAREHEMU AUNT LULU WAAGWA TAYARI KWA SAFARI YA MOSHI TZ

Familia ya marehemu ikiwa imesimama pembezoni mwa mwili wa mama yao mpendwa Lulu Mwaluko aliefariki siku ya Tarehe 7 mwezi wa 3 katika hospitali ya Calvary iliyopo Bronx NY alikokuwa amelazwa kutokana na ugonjwa wa saratani. Watanzania wa New York pamoja na Balozi Tuvako Manongo, Mwakilishi wa kuduma wa Tanzania kwenye Umoja wa mataifa walijitokeza katika kuuaga mwili wa marehemu hapo Camelot Funeral Home Mt Vernon NY.
Watoto wa marehemu mwili huo uliagwa Camelot Funeral Home huko Mt Vernon NY. Mwili wa marehemu utasafirishwa Alhamis kuelekea Moshi Tanzania kwa mazishi.
Mtoto mkubwa wa marehemu akitoa shukrani kwa watu waliojitokeza kuuaga mwili wa mama yao
Mmoja wa familia ya marehemu akiongea 
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania New York bwana Mhella akiongea kwa niaba ya jumuiya
Dr Temba akiongea juu ya jinsi alivyo mfahamu marehemu
Balozi akitafakari jambo
Afisa wa Ubalozi New York Mama Rose alikuwepo sambamba na Watanzania wengine.
Balozi akibadirishana mawazo na Mwenyekiti wa tawi la CCM New York Shekhe Mafutah.
Balozi akipata ukodak kutoka kulia baada ya balozi ni mdogo wa marehemu alitoka Tanzania kuja kumuuguza dada yake.