Tuesday, April 22, 2014

[News] Jaguar ashukuru Wafungwa baada ya video yake kufanya Vizuri.

Baada ya kufanya poa kwa video ya msanii JAGUAR ijulikanayo ka ‘Kioo’. Msanii huyo ameamua kurudi katika gereza la Industrial Area nchini Kenya na kutoa shukrani kwa wafungwa wa gereza hilo kwani video yote ya Kioo ilifanyika ndani ya gereza hilo. Katika video aliyoweka kupitia akaunti yake ya Instagram Jaguar aliwashukuru wafungwa hao akisema “Mnakumbuka ile video tuliifanya apa Kioo? Io ngoma imekuwa kubwa sana na ndo maana nimerudi kusema asanteni sana.”

Jaguar alisindikizwa na Nonini na Bahati ambaye anatamba sana kwa upande wa wasanii wanaoimba Gospel Kenya. Mwisho wa siku Jaguar, Nonini na Bahati walidondosa show ya nguvu kwa wafungwa hao.

Unaweza tazama picha za wasanii hao walipotembelea gereza hilo hapa chini.