Sunday, June 1, 2014

Shadrack Joseph Mnemba (MBETA)

Shadrack Joseph Mnemba (MBETA) 
 
Na : Mwandishi wenu

Katika pilika pilika za kawaida za  Mtandao wako za kusaka habari mbalimbali katika maeneo ya kinondoni Mkwajuni nilifanikiwa kuonana na kijana Shadrack Joseph Mnemba almaarufu kama "Mbeta" akiwa katika majukumu yake ya kila siku ili kujipatia riziki, haikuwa rahisi kwa jicho hili lenye taswira ya uhakika hasa kwa vijana kumpita hivi hivi bila kuongea naye hasa Mtandao wako ulivutiwa zaidi na mwonekano wake na sura yake ambayo inaonekana kufanana kwa kiasi fulani na msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) anayejulikana kwa jina la kisanii "Linex".
       
Mnemba ni msanii wa filamu aliyezaliwa huko mkoani Dodoma miaka kadhaa iliyopita,katika harakati zake za kutafuta maisha, msanii huyu alihamia mkoani dar es salaam huku lengo lake kuu likiwa ni kuja kuungana na wasanii wengine wa fani hii ili aielewe na kujifunza na kuwa nyota wa filamu Tanzania. Haikuwa rahisi sana kama alivyokuwa anawaza kwani alikutana na changamoto nyingi zilizomfanya kutofanikiwa kwa haraka na kumfanya kuwa mmoja kati ya wale wengi wanaohangaikia kufahamika katika sanaa hii.
 "Nilikuja Dar es salaam nikiwa na lengo moja la kuwa mmoja kati ya mastaa wa sanaa hii lakini nilikutana na changamoto nyingi ambazo mbali na kunijenga kiakili pia zimenifanya kuzidisha zaidi juhudi za kutaka kufika mahali ambapo nataka kufika, nilisha wahi kupita katika vikundi mbali mbali vya sanaa na nilifanya mazoezi mengi ya sanaa japo mpaka sasa sijatoka lakini naamini kuna siku nitasimama mwenyewe na ntafanikiwa kuwa mmoja wa wasanii bora wa sanaa hii ya uigizaji" alisema msanii huyo.

Katika kutaka kujua zaidi mtandao wako  ulimuuliza kama alishawahi kukaa mbele ya kamera na kufanya filamu yoyota; Mnemba (Mbeta) aliujuza Mtandao wako pendwa kuwa tayari ameshafanya filamu kadhaa akiwa kama msanii mshiriki katika makundi mbali mbali ya uigizaji, Mbeta alizidi kututanabaisha ya kuwa kwa sasa tayari ameshamaliza kufanya filamu yake mwenyewe inayoitwa "MSUKULE HAI" aliyomshirikisha msanii mkongwe katika tasnia hii ya uigizaji anayejulikana kwa jina la Mzee Magari, ukiangalia katika hilo kava hapo chini huyo anayeonekana kama msukule ndiye "Mbeta" mwenyewe akiigiza kama msukule.
 Hapo juu ndiyo kava la filamu ya kwanza ambayo ameiigiza akiwa mmiliki inayokwenda kwa jina la
"MSUKULE HAI"
 
 Hata hivo kwa mtazamo mpana  Mtandao wako imejibainisha kuwa Shadrack (Mbeta) ni msanii ambaye anahitaji sana msaada wako wa kumsapoti kwenye kazi zake za sanaa kama anavobainisha mwenyewe hapa."Chamsingi naomba sana watanzania waniunge mkono katika kazi zangu za sanaa, pia naomba waniunge mkono pale filamu yangu ya MSUKULE HAI itakapoingia sokoni kwa kuinunua kwa wingi ili harakati zangu zizidi kusonga mbele na ndoto zangu za kuvuka kimataifa zitimie".
Hata hivo msanii huyu aliutanabaisha Mtandao wako ya kuwa katika harakati zake za kusaka ridhiki hajaishia tu kucheza filamu pia anaweza, kuimba Muziki na kucheza Ngoma za kitamaduuni pamoja na kufanya maonesho ya Kula moto, kwa wasanii mbali mbali ambao watapenda kumshirikisha katika kazi zao au kujua zaidi kazi zake, mtaweza kumpata kwa mawasiliano ya namba hizo hapo chini. nk.
 
+255 713 254553
+255 767 254553
Email: mbetasm@