Saturday, November 22, 2008

Kanyama Chiume 11/22/1929-11/21/2007

Dad it has been a year since
You closed your eyes forever.
A year of sadness,
A year remembering the
Good memories we shared together
And a year of hoping the angels
Above are protecting you.
Dad we miss you every day, every hour,
Every minute, and every second.
Hoping one day we shall meet again.
May you rest in peace

Your loving family.

Kanyama Chiume

I see your smile
A mile far away
I see your face
Bearable to stress
I hear your jokes
I remember your hopes
No matter how long it took
You always wished the best
Rest in Peace!
Love you always daughter JMC


1 comment:

  1. Nimeyahariri kidogo yale niyotundika tarehe 26 Novemba 2007 kwenye mjengwa.blogspot.com kwa jina la uandishi “Born Again Pagan” katika kuomboleza kifo cha Mzee Kanyama Chiume.

    Ujumbe wake una maana zaidi katika nyakati za kumkumbuka Mzee Kanyama Chiume aliyetuacha. Naomba mniruhusu niyatundike tena hapa bloguni:

    ODE to Kanyama Chiume - 11/22/1929-11/21/2007 (Kiswahili)

    Kanyama Chiume mahali pema peponi
    Muumba aiweke roho yako;
    Ewe mtoto mpendwa wa Afrika,
    Ewe mtoto mpendwa wa Malawi,
    Ewe mtoto mpendwa wa Tanzania,
    Kwa yale uliyokipigania,
    Hadithi (legacy) yako
    Itabaki siku zote!

    Mzee Kanyama Chiume (RIP)
    Tuliobakia sisi twakuombea
    Bila woga wala simanzi
    Upumzike kwa amani;
    Walio karibu na hiyo “nyumba”
    Wakimiruzi vita kali uliyopigana
    Wapalilie ziotazo nyasi;
    Na wayalinde mema uliyopanda
    Ya kumkomboa m-Afrika mlalahoi!


    Miti uliyoipanda Malawi
    Miti uliyoipanda Tanzania
    Ya yote mazuri,
    Hususan watoto wako,
    Ziunganishe Tanzania na Malawi
    Siku zote ibakie "legacy" yako
    Na kila tukukumbukapo = Kwacha!
    Mzee Kanyama Chiume (RIP)
    Pumzika Mzee: nzuri kazi uliofanya!

    -----------------------------------

    Kifo cha Mzee Kanyama Chiume (mmojawapo wa “ngwazi” hasa wa “Nyasaland” - baadaye Malawi) ni pigo kubwa kwa Afrika nzima (kutokana na darubini ya Pan-Africanism), Malawi na Tanzania.

    Wengine watajiuliza kwa nini namhusisha Kanyama Chiume (marehemu) wa Malawi na Tanzania? Jibu: Maisha ya Kanyama Chiume yalijikita sana Tanzania.

    Moja , miaka ya ujana wake alikuwa Tanzania. Kanyama alikuja Tanzania (akingali mtoto wa shule ya primari) kuishi kwa mjomba wake aliyekuwa akifanyakazi serikalini. Kasomea huko Ifakara (kama sikukosea) hadi kuwasili mjini Dar es Salaam kujiunga na Shule ya Kichwele (Uhuru).

    Mbili, kasoma Tanzania. Kanyama Chiume alikuwa ni kijana mwenye akili. Kashinda hapo Kichwele Primary School (Uhuru) Dar es Salaam kujiunga na Tabora School. Alipambana na “kejeli” za wakati huo hapo shuleni baina ya wanafunzi wa “Bara/Nyika” na “Mwambao/Pwani”. Yeye akatokea Dar es Salaam (“Mwambao/Pwani”). Wa-“Bara/Nyika” walikuwa wakiwaita kwa kejeli wa-”Mwambao/Pwani” kuwa ni “Waswahili”.

    Kafunzu kujiunga na masomo ya sekondari. Wakati huo, watoto wa ki-Ulaya na ki-Asia hawakutaka kusoma na wa ki-Matumbi! Watoto wa ki-Ulaya walikuwa wakienda kusoma huko primary huko Kongwa na Dochi (Lushoto) na hapo baadaye kwenda Nairobi na Uingereza, kabla ya kujengwa kwa shule yao ya St. Michael and St. George (Mkwawa). Watoto wa ki-Asia nao walikuwa na shule zao za Aga-Khan, na kadhalika, na wengine walikuwa wakienda kusoma India, Pakistani na Uingereza.

    Lakini kulikuwa na shule za serikali ambazo hazikuwa na ubaguzi. Shule za sekondari (territorial) zenye sifa zilikuwa ni Tabora School (ya serikali kwa watoto wa machifu, wafanyakazi wa serikali wa vyeo vya juu na watoto wa walalahoi wenye akili waliofaulu kushinda Territorial Standard Eight katika Daraja la Kwanza), ikiwa ni pamoja na Pugu (Wakatoliki) na Minaki Waprotestanti).

    Tatu, Kanyama Chiume alidhihirisha kuwa Tabora School ilikuwa na wajibu mkubwa wa kunoa “vichwa” na kufundisha maadili mema maishani. Kawa “kichwa” katika masomo yake (hasa Hisibati). Pamoja na wenzake wachache wakafaulu kujiunga na Makerere University College na kupewa “nondoz” zao (kama mwana-blogu Michuzi anavyoziita) akawa ni Makerereian.

    Nne, kampata mpenzi/mke wa ki-Tanzania na kuzaa naye watoto. Nawakumbuka baadhi ya wa-Malawi wengine walioishi “Tanganyika” ya wakati huo: Oscar Kambona, Michael Kamaliza na Austin Shaba. Hawa walipata nyadhifa za juu ki-siasa na kuwa mawaziri katika serikali yetu. Kanyama hakuwa m-Malawi wa kwanza kuishi Tanzania. Wakati huo ilikuwa rahisi kwa watawala wa kikoloni kuwatafuta wafanyakazi wasomi kutoka makoloni yao ya karibu. Walikuwepo pia wa-Malawi wengine waliopitia nchini kwetu na wengine kuhamia kabisa (Dr. Shaba, Dr. Charles Mtawali, Dr. Kweygr Munthali, John Phombeya, Simpho Msowoya na wakili Sizya) kwa kuwataja baadhi tu.

    Tano, kafundisha Tanzania baada ya kutoka Makerere (Alliance Sekondary School Dodoma) kurudisha ujuzi wa kunoa vichwa vya vijana wa ki-“Tanganyika”. Wengi waliopita hapo enzi hizo wanamkumbuka umahiri wake katika sayansi na hesabu. Wakati wa kupigania uhuru ulipowadia, Kanyama Chiume alifunga virago vyake kurudi “Nyasaland” kutekeleza majukumu matatu:

    Kuunganisha na kuwahamasisha wananchi wa “Nyasaland at the grassroots level” ili kuwatayarisha kwa utaifa wao.

    Kupigania haki ya kuvunjwa kwa Central Africa Federation (Southern Rhodesia -Zimbabwe, Northern Rhodesia –Zambia na Nyasaland- Malawi). Hao wazungu wachache walikuwa na njama za kutaka kuungana na wenzao wa Afrika Mashariki na kuendeleza himaya ya Mwingereza kutoka Cape Town mpaka Cairo ili kicked ndoto ya mbeberu Cecil Rhodes! Kwa bahati nzuri wa-Ulaya ya Afrika ya Mashariki walipinga sera hiyo.

    Kukabili ukoloni wa Mwingereza ili uhuru wa Malawi upatikane kwa misingi ya Pan-Africanism. Kanyama Chiume na wenzake ndio waliomkaribisha Dr. Hastings Kamuzu Banda kutoka “self-exile” majuu ili arudi nyumbani awaongoze katika mapambano ya kuleta uhuru. Lakini baadaye siasa za Rais wao zilikwenda kinyume cha walalahoi wa Malawi.

    Sita, kakimbilia ukimbizini Tanzania. Sera za Dr. banda zilikiuka msimamo wa Afrika dhidi ya tawala za wazungu wachache huko kusini mwa Afrika. Dr. Banda aliungana na hao wazungu wachache, hasa wabaguzi Makaburu wa Afrika Kusini.

    Kanyama Chiume na mawaziri wengine walijiuzulu na kukimbilia nchi za nje. Kanyama Chiume akaja Tanzania pamoja na Orton Chirwa (Wakili Mkuu wa kwanza wa Malawi) na mke wake wakili Chirwa na Prof. G.M.P. Michongwe, kwa kutaja wachache tu.

    Wakati wa siku zangu hapo Tabora School (1964), wanafunzi wawili wa-Malawi walipewa nafasi na serikali yetu wajiunge na Tabora School: Archibald (Kapote) Mwakasungura (Form Five yetu) na Kingston Msowoya (Form Three) kutokana na kuwaunga mkono mawaziri wao waliofukuzwa na Rais Banda.

    Saba, kawa mwandishi wa makala maalumu ya magazeti ya The Nationalist, Daily News na Uhuru/Mzalendo (wakati wa harakati za ukombozi dhidi ya tawala za wazungu wachache huko kusini mwa Afrika) akiwa Tanzania.

    Nane, kawa mpigania uhuru wa Malawi (awamu ya pili) akiwa Tanzania.

    Tisa, kawa mchapishaji wa vitabu (kampuni ya PanAfric) akiwa Tanzania hadi pale hali ya usalama kisiasa ilipobadilika kufuatia kifo cha Rais Dr. Hastings Kamuzu Banda.


    -----
    Mauma

    ReplyDelete