Monday, November 24, 2008

OMBI LA MJADALA
Kuna Watanzania wengi wa jinsia na marika mbali mbali waishio Jijini New York na kwenye vitongoji vyake ambao kwa idadi tungetosha kabisa hata kuunda kamji kadogo, lakini ajabu ni kwamba mpaka wa leo hatujafanikiwa kuunda umoja. Watanzania wenzetu wengi waishio miji mingine na hata nchi mbali mbali duniani kote wamejibiidisha sana katika hili. Nadhani wakati umefika kwa sisi tuishio Jijini hapa kuamka na kutambua ya kwamba "umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu". Tunahitaji kujikusanya na kuunda Umoja wa Watanzania New York, kwa kutambua kwamba tunahitajiana kwenye shida na raha, leo na kesho na hasa hasa ukizingatia kwamba hapa ni ugenini.
Kama mkereketwa nimeonelea nifungue huu mjadala hili nione kama kuna mwenzangu au wenzangu ambao tunalengana kimawazo na kama yuko au wako tayari na hili jambo.
Nawaomba wasomaji wote wa blogu hii mchango wenu katika kuchangia hii mada.
KARIBUNI!!

No comments:

Post a Comment