Wednesday, February 25, 2009


Maisha ya watoto wetu wengi vijijini bado yako nyuma sana. Wengi wa watoto hawa bado hutumiwa kwenye shughuli nyingi za kila siku kama vile biashara, uchotaji wa maji n.k. Uwezakano wa watoto hawa kujikomboa kwa maisha ya baadae ni mgumu sana, hasa ukizingatia ya kwamba hawana msingi mzuri wa elimu. Wengi wao uishia mijini na ndio wengi tunaowaona wakibabaisha maisha mijini. Asilimia kubwa ya Watanzania bado inaishi vijijini na katika hali ya dhiki. Taifa letu kamwe halitaendelea kama hakutakuwa na uboreshaji wa hali ya maisha ya Watanzania vijijini na elimu lazima iwe mkazo wa kwanza.

No comments:

Post a Comment