Wednesday, February 25, 2009

MAMBO YANAYOTUFANYA TUWE WASWAHILI...

1. Unamwita mtu usiyemjua(wala kukutana nae kabla) aunt au uncle ama shemeji.
2. Asilimia 90 ya CD pamoja na cassete za muziki ulizonazo nyumbani ni feki.
3. Stoo yako imejaa vitu(makorokoro) kwa kuwa hutupi kwa kuamini kuwa ipo siku utayahitaji.

4. Una machupa matupu ya maji, shampoo, perfume pamoja na vipodozi vingine umeweka tuu wala huna shughuli navyo.

5. Watoto wako wote wana majina ya utani, mfano babu ali, Chidi, Dida, n.k.

6. Mifuko yako imejaa vitu kama vile vijiti vya kusafishia meno, tissue n.k. ulivyochukua sehemu kama vile mgahawani.

7. Rafiki yako anapokuwa na mgogoro na mpenzi wake unatamani kisiri-siri waachane ili umchukulie shemeji yako, japo unajidai kuwapatanisha kwa bidii sana.

8. Hupigi simu isipokuwa katika muda ambao gharama za kupiga ni nafuu(mfano- usiku sana) na mara nyingine huwa una beep tu.
9. Wakati ukusafiri japo una naulu kamili unatamani konda asahau kukudai ama umlipe pungufu ya nauli ya kawaida.
10. Unapomsaidia mtu na akafanikiwa basi utakuwa unasema kama sio mimi asingekuwa vile yule.
11. Ualikwapo kwenye sherehe au mkutano hufika baada ya muda ulopangwa kupita, na waweza zidisha hata masaa mawili mbele au zaidi.
12.Unapokuwa kwenye sherehe hutaki kuchukuliwa video.

1 comment:

  1. Ndugu Kombo hapo umetonesha kidonda. Kushindwa kuonyesha kuwa tunaweza kutimia majukumu yetu kwa wakati tuliojipangia ni mojawapo ya uswahili. Wengi tukiweka ahadi hatutimizi kwa wakati muafaka.

    ReplyDelete