Thursday, February 26, 2009

Na: Matina Nkurlu

Vodacom Tanzania yasherehekea Foundation Day


Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania jana imesherehekea siku maalumu ya mfuko huo wa kusaidia jamii ( Vodacom Foundation) katika kusherehekea siku hiyo, Mfuko huo wa Vodacom umezikabidhi hospitali za wilaya za mkoa wa Dar es Salaam msaada wa vitanda maalum kwa akina mama wajawazito vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 40.
Msaada huo ulikabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Bw. Dietof Mare kwa Waganga Wakuu wa hospitali hizo.
Baadhi wa waganga hao waliipongeza Vodacom kwa msaada huo kwani utasaidia kuboresha utoaji wa huduma katika hospitali zao.
Hospitali zilizofaidika kwa msaada huo ni Amana (Ilala) ,Temeke na Mwananyamala (Kinondoni) .
Sanjari na utoaji wa msaada huo kwa mkoa wa Dar es Salaam, Vodacom ilitoa misaada ya aina hiyo katika hospitali za serikali katika mikoa ya Kigoma,Iringa,Kagera na Tanga kupitia kwa wawakilishi wake waliko mikoani.
Waganga hao walisema msaada huo ni uthibitisho wa ushirikiano imara baina ya Vodacom na sekta ya afya hapa nchini na kwamba ushirikiano huo umekuwa ukiimarika kadri muda unavyokwenda.
Walisema serikali mara nyingi imekuwa ikiiomba sekta binafsi kushiriki katika kuboresha mazingira ya upatikanaji wa huduma bora za afya hapa nchini, hivyo basi ushiriki wa Vodacom ni sehemu ya mchango wa sekta binafsi kwa maendeleo ya jamii.
"Tumefarijika sana kuwaona Vodacom wanashirikiana katika sekta hii muhimu ya maendeleo ya jamii," walisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietof Mare, alisema Vodacom Tanzania kupitia mfuko wake itaendelea kuiunga mkono serikali katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini.

No comments:

Post a Comment