Saturday, February 28, 2009

Wakati umefika sasa kwa Waafrika kutokuendelea kuwaonea haya viongozi mafisadi ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakiwanyima haki halali za watu wa bara hili. Kwa miaka mingi tumekuwa tukipokea mapesa mengi ya misaada kwa ajili ya maendeleo ya watu wetu lakini badala yake mapesa hayo yamekuwa yakiwatarijisha wachache tuliowaamini kuwaweka kwenye uongozi.


Yanayoendelea Malawi si mageni kwa nchi zetu nyingi barani humu, na Tanzania ikiwa ni mojawapo. Baba wa Taifa letu aliipigia sana kelele rushwa kwa kusema kuwa "RUSHWA NI ADUI WA HAKI", na kutoa au kupokea rushwa ni kosa moja kubwa sana. Sasa iweje bado tuna watu ambao tunajua hawakututendea haki wanacheka na sisi kila siku na sheria zimekaa kimya? Kama kuna tuhuma juu yako basi inapasa tuhuma hizo zijibiwe kisheria. Tukumbuke ya kwamba "panapofuka moshi kuna moto".

Wananchi wa Tanzania wamechoka kusubiri kupata elimu bora, maji safi, huduma bora za afya, mabarabara n.k. Miaka Arobaini na Tatu ya Uhuru ingetosha kutupa vyote hivyo na si kina nanii....wachache ndio wafurahiye matunda ya uhuru.


TANZANIA BILA MAFISADI INAWEZEKANA!! ...... Mliotuibia pesa zetu mzirudishe na mnaofikiria kuiba MKOME.

Fundi Kombo.

3 comments:

  1. Nice post. I learn something new and challenging on websites I stumbleupon everyday.
    It's always exciting to read through content from other authors and practice something from their websites.

    my web page; garcinia cambogia weight loss

    ReplyDelete
  2. Hі there, this weеkend iѕ fastiԁious for me,
    for the гeason thаt thіѕ point in time i am reading
    this fantastic eԁucational artіcle heгe at
    my houѕe.

    my site: dallas plumber

    ReplyDelete
  3. This is a great tip especially to those new to the blogosphere.
    Brief but very accurate information… Appreciate your sharing this one.
    A must read post!

    Here is my website: bet angel

    ReplyDelete